Na Said Mwishehe

IMETIA NANGA! Hivyo ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya meli ya kwanza kubwa kuliko zote tangu nchi ya Tanzania kupata uhuru yenye urefu wa mita 294,kuwasili katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni matokeo ya uboreshwaji wa lango la kuingilia meli na matunda ya Royal Tour.

Akizungumza leo wakati meli hiyo kubwa na ya kuvutia machoni ilipotia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam,Mkurugenzi wa bandari hiyo, Mrisho Mrisho ameeleza imewasili alfajiri ya jana ikitokea katika bandari tofauti.

Amesema meli hiyo imepewa jina la Norwegian Cruise Line Dawn inauwezo wa kubeba watalii au abiria 4700 huku akifafanua kwamba waliokuja nchini ni zaidi ya 2000 na wafanyakazi waliopo ndani ya meli hiyo wakiwa 1000.

Ameongeza kwamba meli hiyo pamoja na kupita bandari mbalimbali kabla ya kuingia Bandari ya Dar es Salaam imetokea bandari ya Mombasa nchini.


''Meli hii imechukua ukubwa wa gati namba 2 na 3.Ujio wake ni historia kubwa na ya aina yake hapa nchini.Ni meli kubwa na mebeba watalii wengi, ujio wa meli hii na idadi kubwa ya watalii ni matokeo mazuri yanayotokana na filamu ya Royal Tour."

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mrisho ni kwamba watalii waliowasili na meli hiyo wanaelekea katika vivutio mbalimbali ikiwemo mbuga ya Selous na vivutio vingine huku akieleza wao TPA wanajivunia maboresho wanayoyafanya katika bandari ya Dar es Salaam.

"Tumeongeza urefu wa kina wa urefu wa mita 14 kwenda chini pamoja na Lango la kuingilia meli ndio tumeweza kupitisha meli yenye ukubwa huo,''amesema.

Ameongeza matarajio yao baada ya maboresho waliyoyafanya ni kuhudumia meli zenye urefu wa mita 305 wanamaratarajio ya hiyo meli.
Sisi matarajio yetu kuhudumia meli zenye urefu wa mita 305.

Amesema wanamshukuru Mkurugenzi Mkuu na Menejimenti kwa maboresho waliyoifanya katika bandari ya Dar es Salaam kwani hivi sasa wanaona matunda yake.

Awali Mkurugenzi Huduma za Meli na Uratibu shughuli za Bandari ambaye pia ni Nahodha Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA),Abdula Mwingamno ameeleza kuwa meli yenye ukubwa huo haijawahi kuingia kwenye bandari yeyote za TPA.

"Kwa kawaida meli kubwa kama hizi uwa tunaingiza nyakati ya mchana ila hii imeingia alfajiri ,maboresho yaliyofanyika yameleta tija kwani hata meli zenye mita 305 nazo zitaingia bila kusuasua,''amesema.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...