BONDIA Hassan Mwakinyo amewatoa shaka mashabiki wa ngumi kuwa pambano lake litapigwa na kuahidi kuwaonyesha uwezo na kutoa burudani .

Mwakinyo anatarajia kupanda ulingoni dhidi ya Mbiya Kanku wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika pambano la mtata mtatuzi litakalopigwa Januari 27 ,2024 katika Uwanja wa ndani wa New Amaan Visiwani Zanzibar

 
Kauli hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa huenda pambano hilo likavunjika tena, kwani kuna baadhi ya watu wamekuwa na nia mbaya humtumia ujumbe mpinzani wake wakimtaka asipigane ili pambano hilo livunjike.

Akizungumza na Wanahabari Leo January 25,2024 bandarini Jijini Dar es Salaam wakati akijiandaa na safari visiwa vya Karafuu (ZANZIBAR)  Mwakinyo amesema amejipanga kuonesha mchezo ambao wengi hawajahi kuuona huku , akiahidi kutoa burudani kwa mashabiki wake.

"Kuna baadhi ya watu wanamtumia meseji mpinzani wangu asikubali kupambana ili pambano liharibike iwe ni kawaida yangu kuharibu pambano tukakubaliana na promota kama itatokea hivyo nitapigana na promota ilimradi watu wapate burudani.

 Amesema amefanya mazoezi kipindi kirefu hivyo ana hamu ya kuonesha kile alichojiandaa, kwani anaamini wengi watafurahia pambano hilo.

Mabondia wengine watakaozichapa katika mapambano ya utangulizi ni
Hemed Pelembela dhidi ya Fikiri Mohammed kutoka Bagamoyo, Hussein Itaba dhidi ya Juma Misumari wa Morogoro,Bakari Bakari na Seleman Hamad,Masoud Khatibu na Yahaya Khamis, Debora Mwenda kutoka mbeya dhidi ya Zulfa Iddi wa Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...