JUMLA ya washiriki 100 wamethibitisha kushiriki mashindano ya 'NBC Waitara Trophy 2024' yatakayoanza Januari 27,2024 katika viwanja vya klabu ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam na Wanahabari leo January 25,2024  Meneja wa Klabu ya Lugalo, Kanali David Mziray amesema shindano hilo la wazi lenye lengo la kumuenzi Waitara litashirikisha klabu zote za Tanzania na nchi za jirani.
 

"Shindano hili limegawanyika katika sehemu mbalimbali watoto, wachezaji wa kulipwa na ridhaa kwa jinsia zote, "alisema Mziray.

Meneja huyo amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kujisajili katika klabu ya Lugalo kwa lengo la kuanza kujifunza kucheza.

"Shindano la mwaka lina majadiliano katika upande wa uboreshaji wa zawadi kwa washindi ambao watashinda."

Kwa Upande wake Mkuu wa Masoko wa benki ya NBC, David Raymond amesema lengo la kudhamini shindano kuendeleza vipaji vya vijana wa mchezo wa gofu.

"Tutaendelea kutoa ushirikiano kwa wadau kwa lengo la kuzalisha ajira za kudumu za muda mchache kwa vijana."


Aidha miongoni mwa Wadhamini wa shindano hilo kutoka Kampuni ya Vinywaji (SBC) Afisa Uhusiano Foti Nyirenda amesema wataendelea kudhamini mashine hayo ya gofu na kuhakikisha mashindano hayo yanajenga mahususi mazuri na kuboresha afya zao kupitia michezo.

Meneja wa Klabu ya Lugalo Gofu Kanali David Mziray akizungumza na Wanahabari Leo January 25,2024 katika Viwanja vya klabu hiyo akitambulisha shindano la Kumuenzi Mkuu wa Majeshi Muasisi wa Klabu hiyo  Mstaafu Generali George Waitara ambapo shindano hilo litafanyika kwa siku mbili na Kufunguwa  January 27,2024 Klabu ya Lugalo jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...