Na. Mwandishi wetu – Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imempongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha fedha kwa ajili ya ukarabati wa vyuo vitano na ujenzi vyuo vipya vinne kwa Watu wenye Ulemavu.

Aidha, Kamati hiyo imesema vyuo hivyo vitatoa fursa kwa wenye Ulemavu kupata mafunzo ya stadi za kazi na huduma za marekebisho.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Fatma Tawfiq leo Januari 16, 2024 Jijini Dodoma wakati wa kikao cha kamati ikipokea taarifa ya utekelezaji wa Mradi wa ukarabati na ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu.

Mhe. Tawfiq amesema Kamati hiyo inatambua mchango wa serikali katika kuthamini Watu wenye Ulemavu, hivyo itaendelea kuishauri serikali kuongeze bajeti kwa kundi hilo ili kukuza ustawi wao.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema Ofisi hiyo itahakikisha inasimamia ubora wa vyuo hivyo ili viweze kutoa mafunzo yaliyo kusudiwa kwa Watu wenye Ulemavu.Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe Mhe. Fatuma Toufiq (kushoto) akieleza jambo wakati wa kikao cha kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa ukarabati na ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu  tarehe 16 Januari, 2024 Bungeni jijini Dodoma.Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi akichangia jambo kuhusu taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa ukarabati na ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu baada ya kuwasilishwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii tarehe 16 Januari, 2024 Bungeni jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja.Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii ikifuatilia wasilisho la Utekelezaji wa Mradi wa ukarabati na ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu ambayo iliwasilishwa kwa kamati hiyo leo tarehe 16 Januari, 2024 Bungeni jijini Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq.Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) akichangia jambo kuhusu taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa ukarabati na ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu baada ya kuwasilishwa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii tarehe 16 Januari, 2024 Bungeni jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi.Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, Rasheed Maftah akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa ukarabati na ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii leo tarehe 16 Januari, 2024 Bungeni jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Katani Katani akitoa maoni kuhusu taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa ukarabati na ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu baada ya kuwasilishwa kwa kamati hiyo tarehe 16 Januari, 2024 Bungeni jijini Dodoma.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu wakifuatilia maoni ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii baada ya uwasilishwaji wa taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa ukarabati na ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi na Marekebisho kwa Watu wenye Ulemavu tarehe 16 Januari, 2024 Bungeni jijini Dodoma.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...