MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Arbert Chalamila leo Januari 25,2024 amewakabidhi Jeshi la Polisi, Jeshi la Uokoaji na Zimamoto na Jeshi la Uhamiaji Vifaa vya kazi kwaajili ya kuendelea kuimarisha Ulinzi na usalama katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo kati ya wadau mbalimbali na jeshi la polisi, amesema kuwa Ulinzi na Usalama katika jiji umeimarika kutokana na kutokuwepo na vikwazo vinavyosababisha mwananchi asiendelee kufanya kazi kwa amani.
RC Chalamila ametoa sababu ya kwanini anagawa vifaa hivyo vya kazi kuwa ni ameangalia usalama wa kanda, Wilaya na mkoa wa Dar es Salaam kwa ujumla.
"Hali ya Usalama imeimarika kwa kiasi kikubwa sana, ila kumekuwa na matukio kadhaa ambayo yamehatarisha hata maisha ya Askari wetu, tusiruhusu hata kidogo raia kukipeleka kidole chake kwenye jicho la Askari yeyote."
Pia ametoa rai kwa wananchi wote kudumiasha amani katika taifa letu wani ndio walinzi wa amani hiyo na wasije wakaingia kwenye katika mtego wowote wa kuona Askari wa aina yeyote ni adui kwenye maendeleo yao.
Mkuu wa Mkoa amesema kuwa aliona kwenye mitandao ya kijamii ikieleza kukosekana kwa usalama kwenye eneo la Tanganyika Pekers pale Kawe na akampigia simu RPC wa Kinondoni.
" Figisu figisu huwa zinakuwepo hata kwenye taasisi za dini na nikamshirikisha Apostle Boniface Mwamposa kwamba na yeye awe sehemu ya kuimarisha amani ya mkoa wetu." Ameeleza
RC Chalamila amesema kuwa amani huwa hailindwi na neno la Mungu tuu, inalindwa kwa nguvu zote ambazo Mungu alizotoa kwa wanadamu.
Vifaa hivyo vya kazi vilivyotolewa ni Pikipiki 10 zilizotolewa na wafanyakazi wa Kampuni ya Bakharesa, Kanisa la kuhani Musa Richard Mwasha lililoko Kimara Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam pamoja na Askofu wa Kanisa la Rise and Shine, Boniface Mwamposa 'Bulldozer'.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...