Na Said Mwishehe, Michuzi TV

SERIKALI ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya nchini na hasa katika huduma ya mama na mtoto kwa lengo la kupunguza vifo vitonavyo na uzazi pingamizi.

Kauli hiyo imetolewa leo Januari 11, 2024 na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila wakati akiwakabidhi  wabunge wa majimbo 10 ya Mkoa wa Dar es Salaam vifaa tiba vyenye thamani ya sh. Milioni 691 vilovyotolewa na Serikali kwa majimbo ya mkoa huo. 

Amesema  vifaa hivyo ni miongoni mwa vifaa vilivyozinduliwa wiki iliyopita na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kwa nchi nzima vikiwa na gharima ya Sh. bilioni 14.9 kwa majimbo na halmashauri  214 nchi nzima.  

"Rais Dk. Samia  amedhamiria kumaliza vifo vinavyosababishwa na uzazi, hivyo uwekezaji mkubwa unaendelea kufanyika katika sekta hiyo, " amesema Chalamila na kuongeza mkoa huo umepewa zaidi ya Sh. bilioni 52 kuimarisha sekta ya afya.

Amesisitiza na wanaboresha kujenga vituo vipya vya afya na kuiwezesha MSD  kusambaza vifaa tiba vya kisasa katika vituo vya umma vilivyo tayari kutoa huduma kwa wananchi.

“Mbali na kupokea vifaa hivi  jiji hili limenufaika na uwekezaji huo mkubwa unaohusisha uboreshoji wa miundombinu, vifaa, utoaji huduma huku utekelezaji wa miradi mingine mipya ukiendelea."

Chalamila amesema uwekezaji huo unaofanywa na Serikali katika sekta ya afya umeleta mapinduzi makubwa ya utoaji huduma hivyo ametoa mwito kwa jamii kuchangamkia fursa ya bima ya afya kwa wote ili kupunguza gharama za matibabu.

Amesema hatua hiyo ya bima ya afya kwa wote hususani kwa wananchi wa hali ya chini itawaondolea mzigo wa kutelekeza maiti kutokana na kukimbia gharama. “Nitumie fursa hii kutoa mwito kwa wananchi tuhakikishe tunawatia moyo watoa huduma wetu...

"Wanafanya kazi kubwa zipo changamoto lakini na mazuri yapo kazi zao ni ngumu sisi hatuwezi, kila mmoja na kazi yake kuokoa maisha ya mtu au kufanya kazi pale chumba cha kuhifadhia maiti si jambo dogo,”alisema.

Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge Mussa Zungu, alimpongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa wabunge wa majimbo yote lengo likiwa kuboresha sekta ya afya nchini.

"Rais Dk. Samia mpaka Novemba mwaka 2023 peke yake amewekeza zaidi ya trilion sita katika afya.Mwezi uliopita kila Mbunge amekabidhiwa gari moja na wabunge wako 528 wamepatiwa gari la kubeba wagonjwa.

" Rais Samia ametoa magari hayo kwa wabunge kwa lengo likiwa kuhakikisha vifo vya mama na watoto vinapungua, "amesema Naibu Spika Zungu huku akiwatumia nafasi hiyo kuwapongeza watoa huduma za afya.

" Niwapongeze wauguzi na madaktari kwa kuendelea kutoa huduma.Kwa kipekee nimpongeze Mganga wa wa Jiji la Dar es Salaam Dk.Mohamed Mang'unya ambaye amefanya maboresho makubwa katika huduma za afya katika Jiji la Dar es Salaam katika kipindi kifupi."

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Boharibya Dawa (MSD) Mavere Tukai, amesema vifaa hivyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali kukabiliana na changamoto ya vifo vya mama na mtoto.

Ameongeza mkakati wa kugawa vifaa hivyo ulizinduliwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ambapo serikali imetumia sh bilioni 14 kununua vifaa hivyo ambavuo vitasambazwa katika halmashauri za wilaya zote nchini.

Kwa mujibu wa Tukai, kwa Dar es Salaam vifaa vyenye thamani ya Sh. milioni 700 vitagawiwa katika zahanati na vituko vya afya vyote mkoani humo.

Akitoa salamu za shukran kwa niaba ya wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Ubungo, Profesa Kitila Mkumbo amesema vifaa hivyo vitaleta ahueni kubwa kwa wananchi hususan kuepuka vifo vya mama na mtoto.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...