Mwanamuziki Mkongwe Sultan Skassi maarufu "Kasambura" akizungumza  machache mara baada ya kutambulishwa katika bendi ya Sikinde OG Jijini Dar es Salaam na kuhadi kuwakonga Mashabiki wa bendi hiyo kwa vibao vikali.

Meneja wa Bendi ya Sikinde OG Juma Mbizo  akizungumza na Wanahabari   juu ya utambulisho wa Wasanii wawili kuongeza nguvu katika bendi hiyo akiwema Mkongwe Kasambura pamoja na Awadh Mbulu.

  Na Khadija Seif, Michuzi blog
BENDI ya muziki wa dansi, Sikinde Original yatambulisha mwamuziki mpya, mkongwe, Sultan Skassi maarufu kama 'Kasambura' alietamba kwa ngoma mbalimbali ikiwemo 'Christina'.

Mbali na kumtambulisha mkongwe huyo lakini wamemtambulisha mwimbaji mwingine igizo jipya upande wa vijana, Awadh Mbulu 'Mbulu Jr' kwa lengo la kuitumikia Sikinde Original.

Akizungumza na Michuziblog Jijini Dar es Salaam Meneja ya bendi hiyo Juma Mbizo amesema lengo la kusajili wanamuziki wapya ni kuongeza nguvu na kuzidi kufanya vyema ndani na nje ya nchi.

"Mwaka huu tumejipanga kufanya mambo makubwa ndiyo maana tumesajili wanamuziki wenye uwezo kubwa, pia hivi sasa wapo mazoezi kuandaa nyimbo tatu," alisema Mbizo.

Meneja huyo ameweka wazi kuwa mwisho mwa mwezi huu watakuwa wameshamaliza kurekodi nyimbo hizo na kuzitambulisha kwa Mashabiki zao.

Mwanamiziki, Skassi amesema amefurahi kuungana na bendi ya Sikinde Original, atahakikisha anashirikiana vyema na wanamuziki mwenzake katika kutoa nyimbo zenye ushindani.

"Nimefurahi kufanya kazi na watu ambao kipindi cha nyuma nilikuwa nao pamoja nitahakikisha nashirikiana nao katika kuendeleza kutoa burudani kwa wadau wa muziki wa dansi," alisema Skassi.

Upande wa Mbulu amesema pamoja ya kuwa kijana lakini watanzania wasubili kuona uwezo wake wa kuimba nyimbo mbalimbali ambazo atapewa kuimba na bendi hiyo.

Pia ameongeza kuwa amejipanga kutoa mikwaju mikali kama sehemu ya kuaminiwa na kupata mashabiki wapya wa muziki huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...