Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inakaribia kumaliza ujenzi wa madarasa 5,000 kuondoa zamu mbili kwa wanafunzi nchi nzima na kubakisha zamu moja.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo alipofungua rasmi Skuli mpya ya Sekondari Tumekuja iliopo Mwembeladu Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 09 Januari 2024 katika shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Vilevile Skuli hiyo mpya ya Tumekuja ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 1,755 kwa wastani wa uwiano wa wanafunzi 45 kwa darasa moja, tayari wanafunzi wameshapangwa wiki ijayo kuanza masomo.

Rais Dkt.Mwinyi amempongeza mkandarasi wa kampuni ya CRJE kwa kujenga Skuli ya kisasa ambayo ina maabara tatu ya kisasa, chumba cha kompyuta, maktaba na ukumbi wa mikutano.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali itaendelea kujenga maghorofa katika sekta ya elimu kwa wanafunzi kutozidi 45 kwa darasa moja .

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amesema Serikali itaendelea kufanya uamuzi sahihi kwa faida ya nchi na kuyakarabati majengo ya mji mkongwe kwani ni urithi wa nchi kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema mafanikio yaliyopatikana katika elimu ni kwa juhudi za Waalimu kwa kuongeza idadi ya ufaulu ikiwemo kutoka wanafunzi 2,000 hadi 6,000 Skuli za Msingi na matokeo ya kidato cha sita ya mwisho ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la tatu kwa asilimia 90.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...