Na. Damian Kunambi, Njombe.

Ikiwa ni msimu wa kuanza muhula mpya wa masomo katika shule mbalimbali kote nchini hali ya kuripoti wanafunzi wa darasa la kwanza na awali wilayani Ludewa mkoani Njombe imeelezwa kuwa ni ya kuridhisha , huku kwa upande wa kidato cha kwanza ikiwa ni ya kusuasua.

Hayo yamebainika baada ya viongozi ofisi ya Mkurugenzi na ofisi ya mkuu wa wilaya Ludewa kugawanyika katika makundi mawili ili kukagua mwenendo wa kuripoti kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza, darasa la kwanza na awali ambapo kundi la kwanza liliongozwa na katibu tawala wa wilaya hiyo Gilbert Sandagila huku kundi la pili likiongozwa na kaimu Mkurugenzi Mathan Chalamila ambapo moja ya sababu iliyoelezwa kupelekea kuchelewa kwa wanafunzi hao ni wazazi kusubiri siku ya Gulio ili waweze kununua mahitaji ya wanafunzi.

Akizungumza mara baada ya ukaguzi huo Kaimu Mkurugenzi Mathan Chalamila amesema ameridhishwa na mapokezi ya wanafunzi hao kwenye baadhi ya shule za msingi huku wakitoa rai kwa walimu na wazazi kuhakikisha wanafunzi wote wanaotakiwa kuanza kidato cha kwanza wanaripoti ndani ya wiki moja ili kuanza masomo.

"Hali ya kuripoti kwenye baadhi ya shule za sekondari bado ipo chini hivyo niwasihi wazazi kuwapeleka watoto wao shuleni kwani kitu pekee ambacho kinaweza kumbadilisha mtoto ni elimu endapo itakuwa kinyume na hapo basi tutatengeneza kizazi cha baadae ambacho hakitakuwa na uelewa na kuwa wazururaji mtaani"

Amesema anampongeza Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kukamilisha miundombinu ya shule kwani kwa sasa shule nyingi zina madarasa bora, majengo mazuri hivyo niwatake wazazi kutii agizo hili.

Naye katibu Tawala Bw. Sandagila amesema maandalizi ya shule ikiwemo vyumba vya madarasa tayari yameandaliwa vyema tayari kwa kuwapokea wanafunzi hao hivyo wazazi wahakikishe wanafunzi wote waliochaguliwa wanajiunga na shule kwa wakati.

" Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na rais wetu Dr. Samia Suluhu Hassan imewekeza pesa nyingi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule ili watoto waweze kupata elimu bora, hivyo niwasihi wazazi wote wawapeleke watoto shule kwani mazingira ni mazuri na haki ya kupata elimu ni haki ya mtoto". Alisema Sandagila


Munawale Swai ni kaimu afisa elimu sekondari na Chrispinus Luoga ni kaimu afisa elimu awali na msingi wa halmashauri hiyo wamesema idara ya elimu msingi na sekondari wamejipanga vizuri kwa ajili ya kuanza mwaka wa masomo huku wakieleza moja ya sababu ya kuchelewa kuripoti kwa wanafunzi hao ni wazazi kutofanya maandalizi ya mahitaji ya watoto wao ya kutosha wakidai kuwa wanasubiri siku ya Gulio ndipo wakanunue mahitaji.

" Walimu wapo tayari, vyumba vya madarasa vipo vya kutosha, rasilimali za ufundishaji zote zipo tunachosubiri ni wazazi kuleta watoto wao mashuleni ili waweze kupata elimu". Amesema Swai







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...