Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi kilichopo Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro kipo katika hatua za mwisho kuingiza tani 500 za sukari katika soko la ndani zitakozaidia kupunguza machungu kwa watumiaji wa bidhaa hiyo ambapo hivi karibuni kumekuwa na vilio juu ya ongezeko la bei sokoni.

Hayo yamebainishwa na Mtendaji mkuu wa Kampuni hodhi ya Mkulazi Bw Selestine Some wakati wa ziara ya kamati ya kudumu ya bunge  ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ilipotembele katika kiwanda hicho kujione hali halisi ya uzalishaji wa sukari ambayo inatajwa kuathiriwa na mvua za Elnino zinazoendelea kunyesha na kuathiri miundombinu ya mashamba na kufanya zoezi la uvinaji wa miwa kuwa gumu.

Some amesema  tayari tani 185za sukari zimefungwa na na tani zengine 300 zipo katika mitambo ambapo zitafanya kufikia jumla ya tani 500 zitakazoingizwa katika soko ili kupunguza changamoto wa upatikanaji wa bidhaa hiyo sokoni.

Aidha Bw Some amesema wanaendelea kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wanaenda kukabiliana na hali ya uharibifu katika miundombinu ya mashamba ili kuhakikisha wanasaidia juhudi za seriakali katika kupunguza changamoto ya sukari nchini.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Deodatus Mwanyika baada ya kujionea hali ilivyo katika kiwanda hicho amepongeza uongozi wa kampuni hiyo kwa kutumia majaribio ya uzalishaji wa sukari kama sehemu ya kupunguza shida za upatikanaji wa sukari kwa wananchi.

Mwanyika alisema licha ya upya wa kiwanda hiko na bado hakijakabishiwa rasmi lakini kipo katika majaribio yenye kuleta tija kwa Serikali na jamii ambazo zitaenda kunufaika kwa kuanza kutumia sukari inayotarajiwa kuingia sokoni Ijumaa ya wiki hii.

Awali akizungumza katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde alielezea mikakati ya Serikali katika kupunguza makali ya bei ya sukari iliyopo sokoni kwa kuanza kuchukua hatua Madhubuti ikiwemo kuagiza sukari tani 100,000 kutoka nje ya Nchi.

Silinde alisema kuwa meli ya kwanza yenye shehena ya sukari kwa ajili ya walaji wa kawaida imeshaingia nchini na ipo tayari kuanza kushushwa bandarini ili kuanza kusambazwa katika masoko na kuuzwa kwa bei elekezi za Serikali.

“Niwahakikishie Wananchi kwa Sukari yote itauzwa kwa bei elekezi  ya Shilingi 2,700 na 3,200. Tunauhakika ikiingia tani laki moja itapunguza kabisa changamoto ya  sukari iliyopo sasa . Alisema Silinde.

Ujenzi wa Kiwanda hicho ulianza Julai 2021 na kutekelezwa kwa ubia kati ya Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa asilimia 96% na Shirika la Uzalishaji mali la jeshi la Magereza  (SHIMA) kwa asilimia 4%

Mtendaji mkuu kampuni hodhi ya Mkulazi Selestine Some akifafanulia jambo juu ya athari za mvua zilivyoharibu miundombinu ya mashamba na kuathiri shughuli za uvunaji katika mashamba ya miwa ya Mkulazi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,  Biashara,  Kilimo na Mifugo Deodatus Mwamnyika
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...