Na.Vero Ignatus,Arusha (Makala Ukatili wa Watoto Mtandaoni)
Wazazi,walezi na jamii kwa ujumla wanalo jukumu kuzunguma na watoto juu ya ukatili wa mtandaoni kwa kuwafundisha namna ya matumizi sahihi ya namna ya kukabiliana na aina tofauti za ukatili na unyanyasaji wa kingono, ikiwepo kurubuniwa pamoja na kuepuka picha,video ,vitabu vya katuni na vingine vingi vinavyoonyesha sehemu za siri za mtoto au kunyanyaswa kingono
Kutokana na watu wengi kuwa na simu janja,saa na vifaa vingine vya kieletroniki wazazi/walezi watambue kuwa ni rahisi ukatili huo kumfikia mtoto mahali popote, hata maeneo salama na yale ya faragha ikiwemo majumbani,shuleni,kwenye basi la shule,hata kwenye nyumba za ibada na hata wakati wa michezo,kwa kurekodi maudhui ya kingono na hatimaye kuyafikisha mtandaoni na kumdhalilisha mtoto.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa wahusika ni watu walio karibu,au wanaowafahamu watoto,uhalifu huo hutendeka wakati mtoto anapokuwa mitandaoni au ana kwa ana , ambapo mtu yeyote mwanamke/ mwanaume kutoka sehemu mbalimbali za dunia wakiwemo wanafamilia wanaweza kuwa wahusika wa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto mtandaoni.
Katika picha Wakili Msomi Mery Mwita:mtoto anahusika kulindwa katika Sheria nyingine ikiwa ni pamoja na sheria ya mtandao kuhakikisha kuwa watu wote wanaomdhalilisha mtoto
Akizungumzia swala la ukatili Dhidi ya watoto mtandaoni Wakili Msomi Mery Mwita amesema mtoto anahaki zote za kibinadamu kama Katiba ya Jamuhuri ya Muungano ya mwaka 1977 inaeleza katika ibara ya 12(2) kwamba kila mtu anastahili heshima, kutambuliwa na kutathiminiwa utu wake,vilevile Ibara ya 13(1) inasema watu wote ni sawa mbele ya Sheria wanayo haki bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupatiwa haki bele ya Sheria
"Ibara hizi mbili zinampa haki mtoto kupatiwa haki na kutetewa pindi haki zinapokiukwa hata hivyo sheria ya mtoto imepewa meno ya kuadhibu watu wote wanaomfanyia mtoto ukatili wowote"alisema Wakili Mery Mwita
Aidha sheria ya makosa ya mtandao 2015 imeweka adhabu ya wahalifu wa mtandao na kifungo kwa watakaobainika kufanya udhalilishaji kwa mtoto kwa kutumia picha za photograpia ambapo adhabu yake ni faini isiyopungua milioni hamsini au mara tatu ya tathamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria au adhabu ya kifungo cha miaka saba au vyote kwa pamoja
Vilevile Wakili Mwita aliongeza kuwa mtoto anahusika kulindwa katika Sheria nyingine ikiwa ni pamoja na sheria ya mtandao kuhakikisha kuwa watu wote wanaomdhalilisha mtoto wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya Dola kwa kufunguliwa Mashtka inapobaina kuwa wamemdhalilisha mtoto.
Pichani ni Daktari wa Afya ya Akili Edner Solomon Mollel kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha
Kwa kutaka kufahamu zaidi juu ya Madhara yatokanayo na Ukatili na unyanyasaji wa kingono kwa watoto mtandaoni, Michuzi Blog iliweza kumtafuta Daktari Edna Solomon Mollel Mtaalam wa Afya ya akili Halmashauri ya Jiji la Arusha anasema japokuwa mitandao hiyo inawafungulia furasa mpya,lakini pia inawaweka kwenye uwezekano mkubwa wa hatari ya kupata madhara ,hivyo wazazi/walezi wahakikishe kuwa watoto wanatumia vyombo vya kijiditali kwa kuwafunza namna ya kuthibiti madhara yanayoweza kujitokeza, uthibiti huo uende sambamba na ruksa ya kuwawezesha watoto kupata manufaa yanatotolewa na teknolojia ya mtandao
"Madhara haya ya ukatili unyanyasaji wa kingono kwa watoto una madhara makubwa ya muda mrefu ya kimwili ,kisaikolojia ,kijamii kitaaluma,na kiafya kwa watoto na vijana ,jambo ambalo linaweza kuwaingiza kwenye utumiaji wa dawa za kulevya ,au kuwa mtatili na kupelekea kuwafanyia wenzake.alisema Dkt.Edna mtaalam wa Afya ya Akili Jiji la Arusha
Utafiti wa Disrupting Harm kuhusu hali ya ukatili dhidi ya watoto mtandaoni unaeleza kwamba karibia asilimia 4 ya wasichana na wavulana wanaotumia mitandao nchini Tanzania wanafanyiwa vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kingono mtandaoni,
Hii inamaanisha watoto wanalazimishwa kushiriki katika shughuli za ngono mtandaoni,ambapo mtu anatoa au anaweka picha bila ridhaa yao ambapo anashinikizwa kushiriki ngono kwa ahadi ya kupewa pesa au zawadi,hii inawakilisha wastani ya watoto 200,000 wenye umri wa mika 12 -17 kadri matumizi ya teknolojia ya simu yanavyozidi kuongezeka idadi inatarajiwa kuongezeka zaidi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...