TIGO ambaye ni mdhamini wa mbio za Km 21-Tigo Kili Half Marathon za Kilimanjaro Premium Lager International Marahon imewaahidi washiriki na mashabiki uzoefu wa ina yake na wa kusisimua wakati wa mashindano haya.

Hatua hii imekuka ikiwa imebaki takriban mwezi mmoja kabla ya mbio hizi kubwa zinazotarajiwa kufanyika Jumapili Februari 25, 2024 katika Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi.

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael amesema mipango yote imekamilika na kwamba wanatarajia washiriki wengi zaidi na mashabiki katika mbio za Tigo Kili Half Marathon.

“Watanzania wengi sasa hivi wanazingatia mazoezi kama sehemu ya maisha na tumeona wengi wakishiriki katika marathon tofauti ikiwemo Kilimanjaro International Marathon ambayo imejizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi,” amesema.

Amesema washiriki na mashabiki wategemee mtandao bora zaidi na wenye spidi ya hali ya juu wakati wa mbio hizo. (Washiriki na mashabiki hupenda kupiga picha na kuchukua video ili kuwatumia ndugu na marafiki na kurusha mitandaoni. Tunawahakikishia uzoefu wa aina yake katika mtandao wetu ulioboreshwa,” amesema.

Amesisistiza kuwa Tigo imekuwa mstari wa mbele katika kukuza na kutangaza utalii kupitia michezo yaani sports tourism na riadha kwa ujumla na jambo hili limewafanya wawe wadhamini wa Tigo Kili Half International Marathon kwa mwaka wa tisa mfulululizo.

Amesema usajili bado unaendelea kwa njia ya Tigopesa kwa mbio zote yaani km 42, 21 na 5. Washiriki wanaweza kupiga *150*01#, kisha kubonyeza 5 LKS, kisha 5 (Ticket) na kufuata maelezo ili kukamilisha usajili.

“Nafasi ni chache mno kwa hivyo natoa rai kwa washiriki wakamilishe usajili mara moja ili kuepuka kukosa namba kwani nafasi zikijaa waandaaji watalazimika kufunga usajili,” alisema.

Wadhamini wa tukio la mwaka huu ni Kilimanjaro Premium Lager- 42 km, Tigo- 21 km Half Marathon, Gee Soseji – 5Km Fun Run. Wadhamini wa meza za maji ni Simba Cement, Kilimanjaro Water, TPC Sugar, TotalEnergies na CRDB Bank. Wabia rasmi ni –KiliMedair, Garda World Security, CMC Automobiles, Sal Salinero Hotel na wasambazaji wakuu ni – Kibo Palace Hotel na Keys Hotel

Mbio za mwaka huu zitafanyika Jumapili Februari 25 katika Chuo Kikuu Cha Ushirika na kuhusisha mbio za Km 42, 21 na 5.

Kilimanjaro Premium Lager Marathon huandaliwa na Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa kitaifa na kampuni ya Executive Solutions limited.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...