Mwanga
Ushirikishwaji
vikundi vya kijamii kwenye matengenezo ya barabara ya Kisangara kwenda
Shighatini wilayani Mwanga umemfurahisha Mtendaji Mkuu wa Wakala ya
Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff.
Mhandisi
Seff amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya hiyo kukagua mradi wa
matengenezo katika barabara hiyo yenye urefu wa Km. 25, unaofanywa na
kikundi maalum cha kijamii kiitwacho Muhako Engineering, kilichopo
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro.
Mhandisi
Seff amesema amefurahishwa sana na ushirikishwaji huo wa vikundi vya
kijamii katika utekelezaji wa miradi katika matengenezo ya barabara
kwani jamii inayozunguka miradi hiyo inapata ajira na kuweza kuinuka
kiuchumi.
Ametumia ziara hiyo, kutoa wito kwa Halmashauri
kuwajengea uwezo na kuhamasisha vikundi vya kijamii ili viweze kufanya
kazi za matengenezo ya barabara ili kufikia asilimia 30 ya bajeti
zinazotengwa kwa ajili ya kazi hizo kila mwaka ambapo kunawawezesha
kuinuka kiuchumi na kuondokana na umasikini.
Naye Mkurugenzi wa
ufundi wa Kikundi cha Muhako Engineering Bw. Stephen Mkeni alimueleza
Mtendaji Mkuu kwamba wananchi katika eneo la mradi wameshirikishwa vyema
kwenye kazi zinazoendelea na hivyo wameweza kupata ajira na kuwawezesha
kujikimu kimaisha pamoja na familia zao.
Wakala ya barabara za
Vijijini na Mijini (TARURA) hushirikisha vikundi maalum katika shughuli
mbalimbali za matengenezo ya barabara ili kuwezesha jamii kukuza uchumi
wao binafsi pia kuhakikisha wanatunza miundombinu inayozunguka maeneo
yao.
Home
HABARI
USHIRIKISHWAJI VIKUNDI VYA KIJAMII KWENYE MATENGENEZO YA BARABARA 'WAMKOSHA' MHANDISI SEFF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...