Na Mwandishi Wetu
WATANZANIA wameshauriwa kulipuuza Tangazo la Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe la kuwataka Kushiriki maandamano Aliyotangaza kufanyika Januari 24 mwaka huu kwa lengo la kuishinikiza Serikali kuzingatia maoni na mapendekezo ya wadau wa uchaguzi nchini.
Hivi karibuni chama cha CHADEMA kupitia mwenyekiti wake Ffreeman Mbowe kilitangaza maandamano ya Amani Bila kikomo Nchi Nzima, hadi Pale Serikali Itakapofanyia kazi Maoni na Mapendekezo ya Wadau kuhusu upatikanaji wa Katiba Mpya na Chaguzi huru na Haki, ambapo alisema maandamano hayo yanatarajiwa kuanza siku ya Jumatano ya Tarehe 24 mwezi huu.
Alisema Maoni ya wadau hao yalitolewa wakati Muswada wa sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge, na Madiwani wa mwaka 2023, Muswada wa sheria ya tume ya taifa ya uchaguzi wa mwaka 2023, na Muswada wa Sheria ya malekebisho ya sheria ya vyama vya Siasa ya mwaka 2023, ilipotolewa maoni Bungeni jijini Dodoma hivi karibuni.
Viongozi hao wa Baadhi ya vyama vya Siasa Mkoani Dodoma wameyasema hayo mbele ya waandishi wa Vyombo mbalimbali vya habari jijini humo, ambapo wamewataka wananchi na wanachama wote vyama vyao kuyapuuza maandamano hayo na kuendelea na kazi zao za ujenzi wa taifa kwa kuwa mchakato bado unaendelea Bungeni.
Akiongea kwenye mkutano huo Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Mkoa wa Dodoma Yohana Mussa amesema, Maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliyoyaita ya Amani Ukweli ni kwamba hayana Baraka na Ndani yake hayatakuwa ya Amani.
"Sisi kama Chama cha ACT Wazalendo na wenyeviti wenzangu tunaamini maoni yetu yatazingatiwa na wabunge kwa kuwa tumeiona nia njema ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake Katika jambo hili, " Amesema.
"Kwanini Sisi Wenyeviti tusema Maandamano haya sio ya Amani?, ni kwa Kuwa CHADEMA kimeacha mchakato halali wa majadiliano na fulsa iliyotolewa na Rais,Samia ya Maridhiano Kisiasa na kujenga umoja wa kitaifa lakini cha kushangaza, MBOWE na watu wake wanataka kuwaingiza watu barabarani kufanya maandamano katika nyakati hizi ambazo taifa letu linahitaji utulivu mkubwa, " Amesema Mwenyekiti huyo
Naye Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF) Stephen Chitema amewaka wabunge kuzingatia maoni yaliyotolewa kikao cha Bungeni, kuhusu mabadiliko ya katiba kwani Jambo hilo ni la muda mrefu na limekuwa likitumia fedha nyingi.
Kuhusu maandamano ya tarehe 24, amesema Freeman Mbowe ameitisha maandamano ya wafuasi wake na wananchi, wakati ambao wananchi wapo mashambani wakiendelea na kilimo,
"Kwa wito huu anataka wananchi watoke kwenye shughuri za kilimo waje mijini kuandamana hii sio sahihi, " Amesema
Amesema Mbowe anaitisha maandamano katika jiji la kibiashara Dsm huku akitambua juhudi zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kufungua frusa za uwekezaji na biashara katika jiji ilo.
"Lengo hapa sio maandamano ya Amani ila ni uharibifu wa juhudi za Mhe. Rais Katika Kuifungua Nchi
"Sisi Wenyeviti wa Vyama Vya Upinzani Tuliopo Makao Makuu ya Nchini Tunampongeza Rais DK. Samia Suluhu Hassan Kwa Uamuzi Wake wa Kupeleka Bungeni Marekebisho ya sheria ya uchaguzi ambapo sasa, kamati ya kudumu ya bunge ya katiba na sheria chini ya mwenyekiti wake Joseph Mhagama imetoa fulsa kwa wadau mbalimbali kutoa maoni yao Hivyo CHADEMA wajue kila mtu atatoa maoni kwa wakati wake.
Amesema kamati ya bunge ilitoa ushirikiano wa kutosha kwa wadau KIASI cha kutosha ilifikia baadhi ya wadau walipewa nafasi Zaidi ya mara moja kutoa maoni yao wakiwamo hawa wanaitisha maandamano.
"Chama cha Chadema na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe imekuwa ni tabia yao kuacha michakato halali na kukimbilia kwa wananchi kujilizaliza, Sisi wenyeviti Imara tunasema hatuungi mkono maandamano hayo na tunalaani kwa nguvu kubwa ukiukaji huu wa maridhiano ya kidemokrasia yalianzishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, " Amesema
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...