Jumla ya Wakufunzi 13  kutoka Taasisi mbalimbali za Usafiri wa Anga nchini wamefaulu kozi namba 23 ya kuwajengea uwezo wakufunzi katika Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC). 

Akizungumza wakati wa kufunga kozi hiyo Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole aliyemwakilisha Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga(CATC) Aristid Kanje amesema lengo la kozi hiyo ni kuwawajengea uwezo wakufunzi ili wanapotoa mafunzo yawe  yenye tija kwa washiriki.

Pia Longole  amewapongeza washiriki wa kozi hiyo kwa juhudi zao zilizowawezesha  kupata vyeti vya kumaliza badala ya vyeti cha kushiriki kozi hiyo vizuri ikiwa na ufaulu mzuri.

Wakufunzi hao wa kozi hiyo iliyoanza Januari 15 hadi  Januari 26, 2024 ni kutoka Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), Shirika la Ndege la Precision, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)  na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Anga (TCAA -CCC).
Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole akizungumza wakati wa kufunga kozi ya Wakufunzi iliyokuwa na lengo la Kuwajengea Uwezo walimu hao kwenye mahafali  iliyofayika katika chuo cha cha Usafiri wa Anga nchini(CATC).
Mkufunzi mkuu wa Kitengo cha Kuendeleza Mitahala (CATC) Neema Senyagwa akitoa utambulisho pamoja na kueleza dhumuni ya mahafali hayo kwa Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole aliyemwakilisha Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) Aristid Kanje katika mahafali ya kozi ya Wakufunzi yaliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam
Mwalimu kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) Dkt. Daniel Kerenge akitoa maelezo kuhusu namna alivyotoa elimu kwa wakufunzi waliohudhulia kozi ya 23 katika chuo hicho wakati wa mahafali ya kozi ya Wakufunzi yaliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam
Baadhi wa Wahitimu wa Kozi ya 23 wakifatilia hotuba ya Mkufunzi Mkuu wa kitengo cha Uongozaji Ndege, Godlove Longole aliyemwakilisha Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga nchini(CATC) Aristid Kanje katika mahafali ya kozi ya Wakufunzi yaliyofanyika katika chuo hicho jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...