Waziri Wa Mambo Ya Nje Na Ushirikiano Wa Afrika Mashariki, January Makamba (Mb.)akizungumza jijini Dar es Salaam leo Januari, 21, 2024 wakati akielezea ziara za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na ujio wa viongozi mbalimbali hapa nchini kutoka Cuba, China na Poland.



ZIARA ZA VIONGOZI WENGINE WA NJE NCHINI WANAOTARAJIWA KUFANYA ZIARA NCHINI TANZANIA

"Nchi yetu inatambua umuhimu wa kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi na mashirika ya kimataigfa ili kukuza maendeleo ya uchumi, biashara, uwekezaji na ushirikiano katika sekta mbalimbali. Katika kutekeleza hilo, tunatarajia kupokea viongozi watatu kutoka China, Cuba na Polland."

Ameyasema hayo Waziri Wa Mambo Ya Nje Na Ushirikiano Wa Afrika Mashariki, January Makamba (Mb.) wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Januari, 21, 2024, wakati akielezea ziara za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na ujio wa viongozi mbalimbali hapa nchini kutoka Cuba, China na Poland.

Amesema kuwa nchi inatarajia kumpokea Mhe. Liu Guozhong Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China na Mjumbe wa Kamati Kuu ya 20 ya Chama cha Kikomunisti cha China kuanzia Januari,  22- 24 ,2024. 

Akiwa nchini, Mhe. Guozhong anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Mheshimiwa Kassim Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mheshimiwa Dkt. Dotto Biteko (Mb.), Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Cuba
Mheshimiwa Salvador Valdes Mesa, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba anatarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia Januari 23-  25, 2024.

Pamoja na mambo mengine, ziara hiyo imelenga kuendelea kudumusha uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Cuba.

Akiwa nchini, Mheshimiwa Mesa anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Akson, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuzungumza kwa simu na Mheshimiwa Dkt. Husein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

Mheshimiwa Mesa atamtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria Nyerere, na atashiriki kwenye mkutano wa wanachama wa urafiki kati ya Tanzania na Cuba, Watanzania waliosoma Cuba na Taasisi ya PanAfrican Movement pamoja na kutembelea kiwanda kinachozalisha dawa ya Biolarvicide cha Kibaha, Pwani.

Poland
Mheshimiwa Andrzej Duda Rais wa Jamhuri ya Poland atakuwa na ziara ya kikazi nchini tarahe 8- 9 Februari 2024. Mheshimiwa Duda atakutana kwa mazungumzo na mwenyeji wake, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lengo la ziara hiyo ni kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kidiplomasia kati ya nchi zetu.

Tanzania na Poland zinashirikiana katika miradi ya maendeleo ya miundombinu, uhifadhi wa wanyama pori, elimu, maji na usimamizi wa mazingira, utalii, biashara na uwekezaji na ushirikiano wa mabunge.

Ziara hiyo inatarajia kuanzisha maeneo mapya ya ushirikiano katika maeneo ya ulinzi na usalama, nishati na gesi, madini, usafir, ulinzi wa mitandao, utamaduni na uchumi wa buluu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...