Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdulaziz Abood ametoa milioni mbili Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga kata ya Mindu Manispaa ya Morogoro katika harambee ya kuchangia vufaa vya muziki katika kabisa Hilo.

Abood amesema Serikali ipo pamoja na viongozi wa dini na kutambua mchango wao katika suala la kudumisha amani happy nchini.

Ameyasema hayo wakati alipohudhuria harambee ya kuchangia vifaa vya muziki katika kanisa hilo la Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga Kata ya Mindu iliyondani ya Jimbo la Morogoro mini.

Aidha Abood amesema Serikali inatambua mchango wa viongozi wa dini hivyo wataendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali maendeleo Ili kuwasaidia wananachi.

Pia Mhe.Abood amemshukuri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kujali wananchi Kwenye sekta ya afya ambapo hivi karibuni ametoa magari ya kubeba wagonjwa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...