Na Humphrey Shao,Michuzi Tv

BARAZA la Ardhi na Usuluhisho la Kata ya Msimbu halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe,limeshindwa kumaliza malalamiko ya ardhi no 04/2024 ya mwaka 2024 ya Bibi wa miaka 70,Mwajuma Samatta mkazi wa msimbu,ambaye alimiliki na kuishi katika shamba hilo takribani miaka 32.

Akitoa maamuzi ya baraza hilo juzi wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani,Mwenyekiti wa Baraza,Mbaga Salvatory alisema wameshindwa kutoa usuluhisho wa kesi hiyo kwa sababu Mlalamikaji Bibi Mwajuma na walalamikiwa Joseph Ninga,Iddi Shomary, Juma Nassoro na Geofrey Mwaliaje kutokubaliana na mlalamikaji juu ya ugawaji wa eneo hilo.

Alisema katika hilo baraza limeamua kutoa shauri hilo katika Ofisi yake na kulipeleka kwa Baraza la Usuluhisho la Wilaya ya kisarawe.

''Usuluhishi umeshindikana hivyo ni vema shauri hili liende ngazi ya wilaya katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huu,''alisema na kuongeza

''Vielelezo vya Mlalamikaji vinaonyesha alinunua shamba hilo mwaka 1992, huku mlalamikiwa wa kwanza inaonyesha shamba hilo alinunua mwaka 1985 ambapo vielelezo vinaonyesha wote waliuziwa na mtu mmoja ,''alisema.

Kwa Upande wake Mlalamikaji akizungumza nje ya baraza hilo,Mwajuma Samata alisema eneo hilo alinunua mwaka 1992 kutoka kwa Salum Lubilanga lenye ukubwa wa hekari 2 na nusu na tangu ameamia katika eneo hilo hajawahi kuona watu wameingia katika shamba lake ila mwaka 2023 ndipo watu wameanza kujitokeza watu wawili tofauti,''alisema

''Mnamo Septemba 29,2023 majira ya saa 4 asubuhi niliwakuta wakulima shambani 3 nikawauliza kwanini wanalima katika shamba langu wakadai wametumwa na Boss Mohammed ambaye ni Ninga waliondoka wale wakulima,''alisema na kuongeza

''Mwezi wa 10 mwaka jana tena akaletwa mtu mwingine Juma Nasoro ambaye na yeye akasema amenunua shamba hilo hilo kutoka kwa Bwana Ninga na yeye alileta wakulima nilienda kushtaki polisi wakachukuliwa,''alisema.

Alisema alipoenda kushtaki polisi aliambiwa awasilishe hati yake ya manunuzi ndipo alipopeleka hati yake aliyouziwa na Lubilanga huku hati ya Ninga aliyesema amenunua mwaka 1985 ilionyesha kununuliwa kutoka kwa Ali Seif lakini hati yake ilibadilika baada ya kuambiwa apeleke tena polisi na kuja na hati inayofanana majina ya mtu aliyewauzia.

Naye Mlalamikiwa wa kwanza,Joseph Ninga alisema yeye alinunua shamba hilo kutoka kwa Salum Lubilanga ilikuwa mwaka 1985 ambapo yeye alinunuliwa na mtu akiwa nje ya nchi.

Alisema wao waliona ni vema wakasuluhisha mgogoro huo kwa kuwapatia wanunuzi walionunua kwa sasa eneo nusu nusu na kama imeshindikana basi shauri liende wilayani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...