Mkuu wa Mradi wa Kijana Nahodha (Youth Captain), Dkt. Tuhuma Tulli akikabidhi vyeti kwa washiriki wa Mradi wa Kijana Nahodha leo Februari 8, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa hitimisho la mafanikio ya tukio la Ubunifu  (Innovation Lab) kwa  vijana wa taasisi tano za Vijana kuwasilisha namna mradi wao unavyofanya kazi.

Na Avila Kakingo, Michuzi TV.
 
KAMPUNI ya Tanz Med inayojishughulisha na kutoa huduma za afya hapa nchini imeibuka kidedea katika Mradi wa Kijana na kujinyakulia  ruzuku shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kuboresha zaidi suluhisho lao la kibunifu katika kipindi cha majaribio ya miezi sita.

Taasisi yao iliojikita kwenye kuangalia namna teknolojia inavyoingiliana na afya ya akili na mtu binafsi anavyoweza kukabiliana na changamoto hiyo  kupitia jukwaa la majadiliano ya pamoja mtandaoni. 

Amesema kuwa Taasisi hiyo ilioonesha uwezo mkubwa katika kutatua changamoto muhimu zinazowakabili vijana wa Kitanzania.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mkuu wa Mradi wa Kijana Nahodha (Youth Captain), Dkt. Tuhuma Tulli leo Februari 8, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa hitimisho la mafanikio ya tukio la Ubuni  (Innovation Lab) kwa  vijana wa taasisi tano za Vijana kuwasilisha namna mradi wao unavyofanya kazi amesema kuwa wanajivunia Washiriki wote ambao wameonyesha nia ya kushiriki katika mradi huo na kwamba vijana wa Tanzania si tu viongozi wa kesho bali pia ni chachu ya mabadiliko chanya ya leo.

"Kupitia mradi wa Kijana Nahodha (Youth Captain) vijana 45,000 kunufaika kupitia taasisi mbalimbali za Kibunifu za Vijana kutoka Mikoa yote mitano ya Zanziba na Mkoa wa Dar es Salaam na Morogoro." Amesema

Amesema mradi huo unalenga kuwawezesha vijana wa Kitanzania kwa kupata mafunzo, atamizi (mentorship), na ufadhili wa mradi.

"Taasisi za Kibunifu tunazozitaka ambazo zitasaidia vijana na zitazokuwa endelevu na hata taasisi nyingine zinaweza kuchukua ubunifu huo kuuendeleza na kuweza kusaidia Vijana wengi zaidi nchini." 

Dkt. Tulli amesema kuwa Mradi huo unalengo la kusaidia vijana kujiajiri na waweze kuajiriwa pamoja na kuwaunganisha na Makampuni, taasisi mbalimbali kwaajili ya kuwapatia nafasi vijana wabunifu. 

Amesema kuwa Mradi huo utawezesha vijana wa Kitanzania kupitia suluhisho bunifu zinazolenga kuboresha ustawi wao wa kijamii, kujumuishwa kiuchumi na afya.

Awali akielezea mradi huo, Dkt. Tulli amesema kuwa Vijana 120 walijitokeza ili kushiriki katika mradi huo lakini mchujo ukafanyika kupitia Serikali na T-MARC na kupata kampuni tano ambazo zinamawazo bora ya kibunifu na yanasaidiaa vijana kwa wingi.

Dkt. Tulli amesema kabla ya tukio hilo mashirika matano yalichaguliwa kati ya zaidi ya mashirika 120 ambayo yaliotuma maombi, na kupatiwa mafunzo/muongozo kwa muda wa miezi sita iliyopita yaliyolenga kuwawezesha kuboresha bunifu zao.


Kwa Upande wa Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Dkt. Gunini Kamba ametoa wito kwa Vijana kuchangamkia fursa pale zinapojitokeza kwa fursa kwa vijana wabunifu nchini zinafatiliwa kwa ukaribu. 


Kwa Upande wa mshiriki katika Mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Green Composting,  Cecil Sagawa ametoa rai kwa vijana kuwa wabunifu kwa sababu wanaweza kujipatia fursa zitakazo wajengea  uwezo na kupata ajira na kujipatia kipato cha kila siku. 

"Vijana gukitafuta kitu ambacho tunaweza kufanya vizuri zaidi ya vingine tunaweza kuwekeza muda wa kujifunza zaidi ili kufanyavizuri zaidi hii ni njia pekee ambayo vijana wanaweza kujikwamua zaidi kiuchumi." Ameeleza
Mkuu wa Mradi wa Kijana Nahodha (Youth Captain), Dkt. Tuhuma Tulli akizungu leo Februari 8, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa hitimisho la mafanikio ya tukio la Ubunifu  (Innovation Lab) kwa  vijana wa taasisi tano za Vijana kuwasilisha namna mradi wao unavyofanya kazi.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Mkuu wa Mradi wa Kijana Nahodha (Youth Captain), Dkt. Tuhuma Tulli leo Februari 8, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa hitimisho la mafanikio ya tukio la Ubuni  (Innovation Lab) kwa  vijana wa taasisi tano za Vijana kuwasilisha namna mradi wao unavyofanya kazi amesema kuwa wanajivunia Washiriki wote ambao wameonyesha nia ya kushiriki katika mradi huo na kwamba vijana wa Tanzania si tu viongozi wa kesho bali pia ni chachu ya mabadiliko chanya ya leo.














Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...