Katibu Mkuu UVCCM Taifa Faki Rafael Luandala akisaini kitambu cha maombolezo nyumbani kwa Hayati Edward Ngoyai Lowassa  kijijini kwao Ngarash wilaya ya Monduli mkoani Arusha ambapo maziko yake yanatarajiwa kufanyika Februari 17,2024
Katibu Mkuu UVCCM Taifa Faki Rafael Luandala akizungumza na waandishi wa habari akielezea kazi alizozifanya Marehemu Lowassa enzi za uhai wake ambapo amesema watayaenzi mema yote aliyowaachia 
Maandalizi Kwaajili ya Mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Ngoyai Lowasa yakiendelea nyumbani kwake Monduli hao ni baadhi ya Maleigwanan wakiwa kwenue kikao chao cha kimila jamii ya wamasai
Hawa ni baadhi ya Malaigwanan wakiwa msibani nyumbani kwa Marehemu Lowasa kijijini kwake Ngarash wilaya ya Monduli Mkoa wa Arusha 
Pichani ni Laigwanan Mkuu wa Jamii ya Wamasai Tanzania Aisack Lekisongo Meijo :Lowassa ni zawadi tuliyopewa na Mungu katika jamii ya Wamaasai wilaya ya Monduli pamoja na wilaya 14 ambazo wanaishi wamasai hapa Tanzania 
Ni utaratibu uliopo kwa Malaigwanan wa Jamii ya Kimaasai kuwepo na huzuni ama furaha wanapomaliza kikao wanapata chakula ambacho ni nyama kama inavyoonekana kwenye picha, wakiongozwa na Laigwanan Mkuu. 
Katika picha ni baadhi ya wanafinzi wa chuo kilichopo wilayani Monduli bacho kimekuwa kikisapotowa ma Marehemu Lowasa pamoja na Watu mbalimbali wakiwasili nyumbani 
Maandalizi mbalimbali yakiendelea Monduli

Na.Vero Ignatus,Arusha

Leigwanan Mkuu  Aisack Lekisongo Meijao mkuu Jamii ya Wamasai Tanzania ni Mungu alitupati Lowassa kama kwani alikuwa msaada mkubwa kwetu, kama inavyofahamika jamii ya wamasai wanaishi katika mikoa 14 Tanzania na wengi wao wakaendelea kujifunza na kupenda kusoma baada ya yeye kuiomba serikali kuipa jamii hii kipaumbele haswa katika masuala ya Elimu.

"Lowasa aliitambua jamii ya Wamaasai ina umasikini mkubwa hivyo yeye aliamua kuiomba serikali hamii hiyo ipewe kipaumbele haswa kwenye masuala ya Elimu kwa wale waliomaliza kidato cha nne kujiunga na chuo cha waalimu hadi sasa wengi wao wanawafundisha watoto na wajukuu zetu" 

 Kutokana na changamoto iliyokuwa ya maji katika wilaya ya Monduli Hayati Lowassa aliweza kupambana na kuitafuta Benki  ya dunia ikafadhili mradi wa kuleta maji (W) ya Monduli, alipokuwa. Mbunge pamoja na nafasi ya Waziri Mkuu aliweza kupambania wafugaji wa jamii hiyo  na kuhakikisha kuwa Sehemu za Malisho zinatengwa kwaajili ya mifugo.

Meijo amesema kuwa hayatiLowassa wao kama viongozi wa jamii ya wamaasai wanasema kuwa hajafa bali amelala,,amesema Edward alikuwa Leigwanan ambapo yapo majina ambayo waliweza kumpatia ikiwemo IRMAKAA,ILKLSHIMU,ILTOIP hii yote ni kutokana na kushiriki shughuli zote za kimila kwa heshima kubwa na alikuwa hana ubaguzi jamani kwetu ni pengo kubwa,lala Shujaa.

Akimzungumzia Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Katibu mkuu wa UVCCM Taifa Faki Rafael Luandala  amesema  wao kama   wao kama Vijana wa Chama cha Mapinduzi msiba huo kwao ni mkubwa na wamepata pengo kwani marehemu aliwahi kuwa  mmoja wa viongozi wa vijana wa chamanhicho pamoja na Mwenyekiti wa baraza la wadhamini

"Mzee wetu Lowassa alikuwa mtu wa haki mwenye sauti ya Mamlaka hakuwa na ubaguzi alikuwa hakubali kushindwa,ametufundisha kuwa mpole wakati mwingine kujifunza kunyamaza bila kujibu kwa harakapamoja na kuwa na subira kubwa ''alisema Luandala

Amesema kuwa  Marehemu Lowasa  Mwaka 1995 Lowassa alishinda Ubunge wa Monduli kisha mwaka 1998 aliteuliwa na Rais Mkapa kuwa Waziri wa nchi Ofisi ya Mkamu wa Rais  akihusika na Mazingira na kupambana na Umaskini huku ukizingatia kuwa ametokea katika jamii ya wafugaji ya Kimaasai mkoa wa Arusha 

Aidha  Luandala alisema Jina la Lowassa lilianza kufahamika zaidi  baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha kimataifa cha mikutano Arusha, (AICC) na baadaye kuteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Uongozi wa Rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi.

"Kama tunavyofahamu Lowasaa alikuwa hapendi iabisa umasikini ni jambo alikuwa analipiga saba vita hivyo yeye alikuwa chachu ya kuanzishwa kwa Vijana Haouse iliyopo Upanga Dar es salaam ambayo imekuwa msaada kwa vijana kwa kuingiza fedha.alisema

Kwa Upande wale Leigwanan wa wilaya ya Monduli Olebok Leksamba amesema kwamba walipopata taarifa ya msiba ya Leigwanan  mwenzao walisikitika sana ameseama hawawezi kumlaumu Mungu ,amesema kwao wataendelea kumkumbuka kwa kuanzisha shule za kata,na mambo mengi ya kimaendeleo,ametuelimisha ametufundisha mambo mengi namna ya kukaa na jamii nyingine tofauti,hakuna miradi iliyolala kwa kipindi chote alichokuwa kiongozi (wilaya ya monduli ina kata 20)

''Yeye ni Leigwanan rika ya Irmakaa atapewa heshima zote zinazostahili,hakupenda umasikini,alitusaidia kuondoka kwenye nyumba za nyasi na kuingia kujenga nyumba za bati,alikuwa anatusisitiza kupeleka watoto shule sekondari za kulala,kujenga shule za msingi vijijini,,unajua jamii yetu wanapenda kuhama ila yeye alitusisitiza mara kwa mara na watoto wetu waliingia shule hadi sasa wanaendelea kusoma 

Amesema kuwa wananchi wa Monduli hawataweza kusahau suala la maendeleo aliyowafanyia wilayani hapo,katika kipindi cha uongozi wake waliweza kupata bwawa kubwa la maji linaloitwa Oltukai Kijiji cha Oltukai kata ya Isilalee suala la maji lilikuwa gumu Marehemu aliweza kutuwezesha wananchi wa eneo hilo kupata maji

Vilevile amesema kuwa amekuwa chachu ya maendelo kwani alipokuwa mbunge mwaka 1995,alipeleka miradi ya maendeleo ya vijana kwa kupeleka mashine za kusaga,ili kubadilisha uchumi wa kimasai kutoka kwenye ufugaji na kuingia kwenye miradi mingine,aliweza kuanzisha miradi ya mikopo kwa vijana,ambapo vijana walikuwa wanakopepeshwa na kurejesha na wengine wanaingia kwenye mzunguko 

''Imetoka kwenye miradi ya vikundi akaweza kushawishi mabenki kukopesha wafugaji kwa dhamana ya mali walizonazo ambayo inafanyika hadi sasa na imeleta mabadiliko katika jamii ya wafugaji hadi sasa,naweza kusema alikuwa na busara na hekima na alikuwa anajali wadogo hadi wakubwa,alikuwa mchapakazi''

Aidha mwili wa Marehemu Edward Ngoyai Lowassa unatazamiwa kusafirishwa siku ya kesho kutoka Jijini Dar es salaam kuletwa arusha kwaajili ya maandalizi ya Mazishi februari 17 Kijijini kwao Ngarash wilaya ya Monduli.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...