“Good Morning”

Hivi ndivyo alivyotusalimu Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa kila alipoingia kwenye  kikao chochote cha kikazi, iwe asubuhi iwe mchana au usiku  alimradi ni kazi, salamu yake ilikuwa 'Good morning'

Alimaanisha kazi inaanza wekeni kila kitu pembeni tufanye kazi. 

 Edward Lowassa, alikuwa kiongozi jasiri, mkweli, mpenda maendeleo na muumini wa kweli wa Muungano na umoja wa Watanzania.

Aliheshimu watu wote bila kujali rika, nafasi au uwezo wa kifedha. Akiwa rafiki yako ni rafiki yako kweli kweli.

Lowassa alikuwa kaka yangu, rafiki yangu na mwalimu wangu na mtu mwenye mchango mkubwa katika safari yangu ya Uongozi.

Namna pekee  kwa Watanzania kumuenzi Lowassa ni kwa kuchapa kazi kwa bidii kwa sababu alikuwa mtu hodari kwa kutetea maslahi ya watu bila kujali wanakotoka, imani zao wala mrengo wao wa kisiasa.Tutamkumbuka kwa mchango wake katika ujenzi wa taifa letu.


Balozi Dk Emmanuel Nchimbi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...