Na Fauzia Mussa, Maelezo

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Hafidh amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeanza kuwatambua wafanyakazi wa afya ya jamii (CHW) kwa vitendo.


Ameyasema hayo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na stahiki za malipo kwa wafanyakazi hao,huko Ofisi za Wizara hiyo Mnazimmoja Mjini Unguja.


Alieleza kuwa taratibu zote za kazi na malipo kwa wafanyakazi hao zinaendelea kufanyiwa kazi na Wizara ya Afya kupitia Idara ya kinga baada ya kurasimishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi kutoka wahudumu wa Afya wa kujitolea (CHV) kuwa wafanyakazi wa Afya ya jamii (CHW) Disemba 16 mwaka jana.


“Kuanzia mwezi Januari ,2024 stahiki za wafanyakazi wetu hawa zitatoka wizara ya afya kupitia idara yetu ya kinga”.alifafanua Naibu Waziri


Aidha alisema kwa kutambua na kuthamini mchango unaotolewa na wafanyakazi hao katika kutoa huduma za Afya kwa jamii Wizara imejipanga kuwaboresha wafanyakazi hao kwa kuwapatia mafunzo ya miezi 6 yatakayoambatana na mitihani ili kuimarisha utendaji wao .


Zaidi ya wafanyakazi 2000 wamerasimishwa kutoka wahudumu wa Afya ya jamii wa kujitolea (CHV) na kuwa wafanyakazi wa Afya katika ngazi ya jamii ( CHW), ambapo awali walikua wakipata stahiki zao kupitia Taasisi ya D-tree.

Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Hassan Khamis Khafidh akitoa taarifa ya stahiki za malipo kwa wafanyakazi wa Afya ngazi ya jamii,huko Ofisi za Wizara hiyo Mnazimmoja Mjini Unguja.


PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...