Na. Vero Ignatus Arusha

Wizara ya Fedha imeandaa kwa Mara ya pili Jukwaa la Kodi na uwekezaji kitaifa litakalofanyika Jijini Dar es salaam February 27-28, 2024 ambalo litajumuisha zaidi ya wadau 800,na mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Elijah Mwandumbya kwamba uzinduzi huo utakwenda sambamba na Sera isemayo Mageuzi ya Sera lengo la kukuza uwekezaji, ukusanyaji wa mapato ya ndani na kuongeza ukuaji wa uchumi.

Mwandumbya amesema kwa Mara ya kwanza Jukwaa hilo lilifanyika Januari 2023 likiwa na lengo la kuandaa bajeti ya mwaka 2023-2024-ambapo inatelelezwa,hivyo maoni yaliyotolewa yalilenga kuboresha mazingira ya biashara nchini, kukuza uwekezaji, kulinda viwanda via ndani, kuvutia uwekezaji, kuongeza ushindani wa viwanda vya ndani na kuongeza mapato ya serikali.

"Maeneo yaliyofanyiwa maboresho kutokana na maoni yaliyotolewa ni pamoja na kusajili wafanyabiashara katika kundi la. Ukusanyaji wa mapato, ambapo kima hicho kilikuwa milioni 100 Ila kwa sasa kima hicho kita kuwa milioni 200 hivyo mfanyabiashara mwenyekito kiwango hicho anapaswa kujisajili kwenye Kodi la ongezeko la thamani VAT. "Alisema.

Sambamba na hayo Mwandumbya amesema mabadiliko mengine yalifanyika kupitia Bunge,ambayo yamewezesha kukuza biashara kuwa katika maoni yaliyoyapokea yamewezesha kukuza biashara nchini, hali hiyo imepelekea serekali kukusanya kiwango kilivunja rekodi cha shilingi Trillion 3 desemba 2023

Aliendelea kusema waliweza kupokea maoni yaliyopelekea kusamehe Kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye uuzaji wa nyumba Mpya zenye thamani isiyozidi milion 50,pamoja na kusamehe Kodi kwenye vifaa vya kubadilishia vifaa vya Matumizi ya magari kutoka kwenye mafuta kwenda kwenye gesi au umeme ili kuendana na hali ya tabianchi inayoendelea kwa sasa ili kukidhi mahitaji ya soko

Aidha Wizara inajiandaa na Matumizi ya bajeti ya 2024-2025, katika Kuboresha suala la kupokea maoni kwa Watanzania na wadau mbalimbali katika Kuhakikisha wanapokea maoni wakiwemo wafanyabiashara, mabalozi wadau katika serikalini, Sekta binafsi ndani na nje ya nchini, ambapo watajumuika kujadili mustakabali wa uwekezaji nchini, ulipaji Kodi na ukusanyaji wa mapato na namna ya kuboresha mazingira.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Elijah Mwandumbya akizungumza na waandishi wa habari Jijini Arusha juu ya uzinduzi wa pili wa Jukwaa la Kodi na uwekezaji kitaifa utakaofanyika Jijini Dar es salaam February 27-28 2024.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...