Na Janeth Raphael - MichuziTv
KAMATI ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo, Mifugo na Uvuvi imeipongeza Tume ya Ushindani (FCC) kwa kuendelea kudhibiti bidhaa bandia nchini.
Pongezi hizo zimetolewa leo Februari 11,2024 na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe.Deo Mwanyika mara baada ya kupokea wasilisho la utendaji kazi wa FCC bungeni jijini Dodoma.
“Kamati tunapongeza hatua zinazochukuliwa na Tume hiyo katika kudhibiti bidhaa bandia kwa kushirikiana na taasisi zingine na kuwaasa watanzania kuendelea kutoa ushirikiano ili kuondoa bidhaa hizo.”amesema Mhe.Mwanyika
Hata hivyo Mhe.Mwanyika amesema kuwa kamati hiyo itaendelea kutoa ushauri kwa serikali ili kufikia maono ya Rais ya kuchochea uchumi na kuongeza wawekezaji nchini.
“Tunashauri sheria ile iliyounda Tume hii ifanyiwe maboresho kutokana na maeneo mengi teknolojia imebadilika na idadi ya wawekezaji wa ndani na nje imeongezeka tangu Rais Samia ameingia madarakani,”amesema
Naye, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaudi Kigahe, amesema Tume hiyo inapanga kusaidia kudhibiti biashara feki kwa kuwa bado kuna changamoto kubwa inahitajika kufanya kazi ya ziada.
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Bw.William Erio,amesema kuwa wamekutana na Kamati hiyo kuwaeleza majukumu ya tume pamoja na kuwapa mawasilisho yanayuhusu utendaji kazi wa Tume hiyo.
Bw.Erio amesem kuwa Tume imepewa jukumu la kudhibiti uingizaji wa bidhaa bandia, kuzuia uzalishaji wake, kusambazwa au kupitishwa nchini kwenda nchi jirani.
“Tunashirikiana na Brela zile bidhaa zilizosajiliwa mtu asiende kutengeneza zikaonekana kama bidhaa halisi kumbe sio, tumeanza kutoa elimu watu waelewe madhara ya bidhaa bandia kwa kuwa zinaikosesha serikali kodi, zinafanya wafanyabishara halali kufunga biashara zao kwa kushindwa kushindana na bidhaa bandia,”amesema Bw.Erio
Aidha amesema wameiambia kamati hiyo maeneo yenye mlengo wa kisheria yanayopaswa kuboreshwa ili kuongeza ufanisi kwenye utendaji kazi, tumewasilisha serikalini na mchakato umepita ngazi zote za serikali sasa unakwenda ngazi ya bunge ili kubadilisha sheria ya ushindani ambayo ilitungwa mwaka 2003.
MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) BW.William Erio,akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kutoa Semina kwa kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo ,Mifugo na Uvuvi ya kuwajengea uelewa wabunge kuhusu utendaji kazi wa Tume ya Ushindani (FCC) iliyofanyika leo Februari 11,2024 bungeni jijini Dodoma
MKURUGENZI Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) BW.William Erio ,akiwasilisha mada kwa kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo ,Mifugo na Uvuvi wakati wa Semina ya kuwajengea uelewa wabunge kuhusu utendaji kazi wa Tume ya Ushindani (FCC) iliyofanyika leo Februari 11,2024 bungeni jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe Exaudi Kigahe, akichangia jambo wakati wa semina ya kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo ,Mifugo na Uvuvi ya kuwajengea uelewa wabunge kuhusu utendaji kazi wa Tume ya Ushindani (FCC) iliyofanyika leo Februari 11,2024 bungeni jijini Dodoma
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...