NA BALTAZAR MASHAKA,NYAMAGANA

JUMUIYA ya Umoja wa Wanawake (UWT) Tawi la Mwananchi wilayani Nyamagana,mkoani Mwanza,imeadhimisha miaka 47 ya CCM kwa zawadi kwa watoto na kuwaasa wanawake wakiwemo wanawaume kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita za kuboresha sekta ya afya.

Rai hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa UWT, Elizaberth Magiri, wakati akizungumza na akinamama katika zahanati ya Mahina ambapo walikabidhiwa zawadi mbalimbali za watoto zikiwemo sabuni.


“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,ni mama mlezi wa jamii,tunapoadhimisha miaka 47 ya CCM tunajivuna amefanya makubwa ikiwemo kuboresha huduma za afya na huduma zingine zinazidi kusogea ili kuwasaidia akinamama,watoto na wazee,”amesema.

Elizabert amewataka wananchi wa Mahina kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu 2025,wajitokeze kushiriki na wanawake wasimsahau Rais Dk.Samia, wampe miaka mitano tena ili kumlipa fadhila kwa kazi kubwa aliyofanya ya maendeleo.

“Pia,ukimuelimisha mwanamke umeelimisha jamii yote,hivyo akina mama mfahamu madhara ya ugonjwa wa kipndupindu mkuchukue tahadhari zote na kujitahidi kuwa wasafi wa mazingira na watoto wasile vyakula bila kunawa,”amesema

Kwa niaba ya akinamama wenzao,Prisca Benson aliishukuru UWT kwa zawadi za watoto pamoja na Rais Samia kwa kuboresha huduma za afya sasa wanapata huduma nzuri za matibabu zinazotolewa katika zahanati ya Mahina huku Rehema Daniel akiishukuru serikali kwa kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto.

Kwa upande wake Diwani wa Mahina (CCM),Alphonce Francis amempongeza Rais Dk.Samia kwa namna alivyomwaga fedha nyingi za miradi itakyowahudumia wananchi wa kata hiyo na kuwaomba wananchi waiunge mkono serikali katika eneo hilo la miradi.

Ameeleza huduma za afya zinazotolewa katika zahanati ya Mahina hazikidhi kulingana na idadi ya wananchi zaidi ya 50,000,ndio maana wanahitaji kituo kikubwa cha afya kwani azma ya serikali kila kata iwe na kituo cha afya.

“Tunataka wananchi na akinamama wafahamu nini serikali yao inafanya,tumepokea mradi wa jengo la upasuaji,litakapokamilika tunakwenda kutatua changamoto za afya wananchi wapate huduma nzuri karibu na jengo la wagonjwa wa nje (OPD) tayari limefikia asilimia 86 kukamilika na kuiwezesha Zahanati ya Mahina kuwa na hadhi ya kituo cha afya,”amesema.

Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo,Magembe Ng’walida amesema inahudumia wagonjwa 40 na wajawazito wanaojifungua 10 hadi 20 kwa siku, wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji hali inayozorotesha utoaji wa huduma,wanalazimika kununua ndoo ya maji kwa sh.500 nje ya bajeti wakati mahitaji ni ndoo 10 kwa siku.

Amesema jengo la OPD linalojengwa na TASAF litasaidia wagonjwa na kurahisisha utoaji na upatikanaji wa huduma ambapo huduma zote zitapatikana eneo moja badala ya kumsafirisha mgonjwa eneo jingine ingawa wanakabiliwa na uhaba wa viti,meza na dawati la wagonjwa.




Diwani wa Mahina (CCM) Alphonce Francis wa pili kushoto,akizungumza na akinamama (hapo pichani) katika zahanati ya Mahina leo,wakati UWT Tawi la Mwananchi wilayani Nyamagana walipotembelea zahanati hiyo kugawa zawadi kwa watoto,wa kwanza kushoto ni Mganga Mfawidhi wa zahanati hiyo,Magembe Ng'walida.
Wakinamama waliopeleka watoto wao kliniki katika zahanati ya Mahina wakimsikiliza Diwani wa Mahina (CCM) Alphonce Francis (hayupo pichani, leo alipoongozana na Mwenyekiti wa UWT Tawi la Mwananchi kugawa zawadi kwa watoto.
Lawrencia Machunda (kulia) kwa niaba ya akinamama na watoto wao akipokea boksi la vinywaji laini (juice) kutoka kwa Mwenyekiti wa UWT Tawi la Mwanza, zawadi hizo imetolewa na jumuiya hiyo ikiadhimisha miaka 47 ya CCM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...