Na Pamela Mollel,Burigi- Chato

Hifadhi ya Taifa ya Burigi -Chato,imepanga kutoa jumla ya madawati 605 katika shule zenye mahitaji katika vijiji ambavyo vipakana na hifadhi hiyo .

Msaada huo wa madawati Hayo yenye thamani ya sh 42 milioni ni sehemu ya miradi ya ujirani Mwema ambayo inayotekelezwa na hifadhi hiyo Katika wilaya Tano ambazo hifadhi hiyo ipo.

Akizungumza na uongozi wa shule ya sekondari Bisibo iliyopo kitongoji cha Bisibo wilayani biharamulo ambayo ni miongoni mwa shule nufaika na mradi huo Afisa mwandamizi kitengo cha mahusiano na ujirani Mwema,Ombeni Hingi ameeleza idadi ya shule watakazo zisaidia ikiwa ni shule zenye uhitaji mkubwa na zinazo zunguka hifadhi.

"Madawati hayo ikiwepo viti na meza vipo kwenye mchakato wa manunuzi kwa wilaya ya biharamuro pekee tunafanya manunuzi ya viti na meza 242 kwa shule 5 za msingi na nyingine za sekondari " alisema

Alisema katika wilaya ya Ngara wanampango wa kupeleka viti na meza 122, wilaya ya Chato viti na meza 241, hivyo kwa mwaka wa fedha wa 2022,2023 wamefanikiwa kutoa kwa jamii jumla ya madawati 605 yenye thamani ya shilingi Milioni 42.

Kwa upande wale mkuu wa shule ya Sekondari Bisibo Namwamini Alice Faresi ameeleza changamoto ya ukosefu wa madawati kwa wanafunzi kuwa ni mkubwa hali inayopelekea wanafunzi kusoma na kuandika wakiwa wamekaa chini, hivyo kushukuru hifadhi ya burigi kwa msaada wa viti na meza na kueleza kuwa bado uhitaji ni mkubwa hivyo kuomba wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia.

"Tuna uhitaji wa meza na viti 300 Tanapa wametusaidia baadhi hivyo bado uhitaji ni mkubwa wanafunzi wanateseka niombe mashirika mbalimbali na taasisi za kiserikali kusikia kilio chetu na kuwasaidia wanafunzi hawa kusoma vizuri" alisema

Naye diwani Kata ya Bisibo Festo Mutatembwa ameeleza elimu inayotolewa na tanapa katika kutunza hifadhi ni kubwa , na jamii zinazo zunguka hifadhi zinapokea elimu ila bado changamoto za kijamii ni nyingi ikiwemo vituo vya afya ,hostel za wanafunzi na hata madawati ya kukali wanafunzi ni changamoto hivyo wadau wautalii wazidi kujitokeza kusaidia jamii zilizopo pembezoni mwa hifadhi.

Edga Piusi na Siliviana Mathayo ni wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Bisibo ambayo ni wanufaika wa msaada huo wameeleza adha kubwa ya kukaa chini wakiwa wanasoma jambo ambalo linawapekelea kupata magojwa mbalimbali ikiwemo fangasi ,matatizo ya iti wa mgongo na homa za mara kwa mara hiyo kuiomba serikali na mashirika kuwatazama na kuwasaidia.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...