Na Said Mwishehe, Michuzi TV

OFISA Mazingira wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Theodory Mulokozi ameeleza uelewa mdogo wa jamii kuhusu masuala ya usimamizi wa mazingira ikiwemo kudhibiti taka ngumu umekuwa ukisababisha kuenea kwa taka hizo katika maeneo mengi.

Pamoja na hayo amepongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali kupitia TAMISEMI pamoja na wadau wengine wanaohusika na mazingira kwa jitihada wanazoendelea kuchukua ili kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama huku akisisitiza wajibu wa kila mmoja wetu kushiriki kikamilifu katika kudhibiti taka ngumu.

Mulokozi ameyasema hayo katika semina ya mafunzo awamu ya pili kwa waandishi wa habari katika uwajibikaji wa taka za plastiki(EPR) yaliyoandaliwa na Asasi ya Human Dignity and Environmental Care Foundation(HUDEFO) yenye lengo la kuwajengea uelewa kuhusu kuandika habari zinazohusu udhibiti wa taka ngumu kupitia mradi wa Extendend Prod.

Akieleza zaidi wakati akielezea sheria ya mazingira, sera, kanuni na miongozo katika kukabiliana na taka ngumu, Mulokozi ametumia nafasi hiyo kusisitiza umuhimu wa jamii kuwajibika kwa nafasi yake kukomesha taka hizo sambamba na utunzaji wa mazingira kwa ujumla.

“Tunawashukuru HUDEFO kwa kuwakutanisha waandishi wa habari kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu masuala mazima yanayohusu taka za plastiki na sheria ya katazo ya mifuko ya plastiki.

“ Ni jambo jema kuwajengea uwezo waandishi wa habari.Kimsingi tunahitaji ushirika wadau wakiwemo waandishi wa habari hasa hasa katika eneo ambalo linaonesha linazorotesha eneo zima la kuhamasisha wananchi katika kupambana na taka za plastiki.

“Ni kweli tangu tangazo la kukataza mifuko ya plastiki limetoka ni miaka mitano lakini tunaendelea vizuri.Tumefanya mapitio na tathimini kuona wapi tumefika , tunaenda vizuri.”

Amesema sheria ya mwaka 2019 imerekebishwa na kwa sasa kuna kanuni mpya ya mwaka 2022 ambayo kimsingi inajaribu kuondoa changamoto zilizopatikana kwenye kanuni ya mwaka 2019.Kwa hiyo ni jambo jema kukutana na waandishi wa habari.

Amesema kupitia mafunzo hayo inawapa ujumbe wa kuona ni namna gani wanaweza kushirikiana na Serikali kupitia TAMISEMI kufikisha ujumbe kwa jamii kwamba sasa ufike wakati kila mtu awajibike katika kukomesha mifuko ya plastiki na taka ngumu.

Aidha amesema kwa upande wa wananchi wahakikishe hawatumii vibebeo na mifuko ambayo imezuia, hivyo mwananchi akiona mtu anazalisha mifuko ambayo haina viwango kama ilivyoelekezwa na TBS basi atoe taarifa kwa mamlaka husika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa HUDEFO Sarah Pima akizungumzia mafunzo hayo amesema wanafahamu waandishi wa habari ni nguzo muhimu na inafanya kazi kubwa katika jamii yetu.

“Hivyo tuko hapa kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu taka ngumu lakini kuelekea kudhibiti wa taka ngumu kwa wazalishaji hasa wa plastiki. Katika mafunzo haya ni awamu ya pili kwani awamu ya kwanza tulianza nao mwaka jana.

“Kutokana na umuhimu wa habari na kazi wanazofanya tumeona waendelee na mafunzo haya ili kwenda kuandika habari zinazohusu kudhibiti taka ngumu hasa katika kuelimisha na uwajibikaji katika jamii.Kwa kufanya hivyo tunaamini wanahabari wataenda kufanya kazi wakiwa tayari wamejengewa uwezo thabiti.”

Amefafanua katika mafunzo hayo watoa mada wamezungumzia kanuni , sera na sheria pamoja na miongozo jinsi gani zinafanya kazi ni wapi hasa pakuanzia unapoandika habari yako , jinsi serikali za mitaa, halmashauri na taasisi za serikali zinavyofanya kazi kufanikisha utendaji , au jinsi gani waandishi wa habari wataandika kuhusu taka ngumu

“Hivyo basi kupitia semina hizi tunajenga waandishi wa habari ambao ni bora na wataandika vizuri lakini sio tu kwa ajili ya kufanya habari za taka ngumu lakini watakuwa na njia nzuri za kufisha ujumbe kwa jamii lakini kuleta mabadiliko chanya kwa jamii zetu,”amesisitiza.

Kuhusu kasi ya kukomesha taka ngumu Sarah amesema amesema kasi ni kubwa hasa katika makundi tofauti na wameona wadau mbalimbali kama Asas zisizo za kiserikali zimeendelea kufanya kazi kwa katika suala hilo.

“Mimi nikiwa mmojawapo ambaye nimekaribishwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kutoa maoni kuhusu sera mpya inayokuja ambayo imeanza kufanyia kazi udhibiti wa taka ngumu.Kwahiyo hii itasaidia kufanya kazi katika weledi unaotakiwa.

“Pia tunaona juhudi za wanahabari katika mnyororo mzima kwasababu masuala ya taka ngumu yanajumuisha mambo mengi , wadau wengi, hivyo tunaona wanahabari wanavyoshiriki katika udhibiti wa taka ngumu.

“Pamoja na jamii kuwa na uelewa mdogo lakini kuna vitu ambavyo vinaendelea kufanyika kwa mfano halmashauri hususa za Dar es Salaam zina siku za usafi, kampeni za usafi , kila mtu ana moto,”amesema.

Amesisitiza wanaona kuna hatua wamepiga na kuna mahali wanaenda , hivyo ni vema wadau wakaendelea kushirikiana katika kudhibiti taka ngumu kwani ni suala linalohusisha wadau wengi na si mtu mmoja.

 

 Ofisa Mazingira Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Theodary Mulukozi akiendelea kutoa mada kwa waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Asasi ya Human Dignity and Environmental Care Foundation(HUDEFO) Sarah Pima akifafanua jambo wakati wa semina ya waandishi wa habari iliyohusu kuwajenge uelewa kuandika habari za taka ngumu hasa taka za plastiki











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...