Imeandaliwa na Idara  ya Habari MAELEZO 


"Tupo hapa kutoa fursa kwa viongozi wa Mkoa wa Iringa kuwaeleza watanzania wakiwepo wananchi wa Mkoa wa Iringa kwamba nini serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kufanya .

"Mpango huu ambao tumeupa jina la Tumewasikia tumewafikia ulibuniwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kupitia Idara yetu ya HABARI-MAAELEZO kutoa fursa kwa viongozi wetu kuwaeleza watanzania mafanikio ya kazi zinazofanyika"

Yamesemwa hayo na Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO  Mobhare Matinyi  Februari  mosi alipokuwa na mkutano na Waandishi wa Habari, Wakurugenzi  na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halimandego.

"Hii ni kwa sababu Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan  anatoa fedha za kutosha na kuzifikisha kwenye
 Mikoa na Halmashauri zetu ili watanzania wapate maendeleo yanayostahili,
amesema Msemaji Mkuu wa Serikali Matinyi. 

Amesema kuwa Rais wetu na Serikali yake, amewasikia watanzania na amehakikisha anawafikia kwa kutoa fedha hizo, fedha hizo zimekuwa zikiwezesha miradi yetu kufanyika ambayo inagusa huduma za kijamii kama elimu ya msingi na sekondari, afya kwa ujenzi wa Zahanati, Vituo vya afya, Hospitali za Wilaya, za Mkoa na pia zile za rufaa katika maeneo ya Kanda.

Matinyi amesema "kwa mfano katika Mikoa ya Nyanda za juu Kusini Hospitali ipo Mjini Mbeya ambayo inahudumia  wananchi wa Mkoa huu wa Iringa" amesema Matinyi.

"Fedha hizo ambazo ni  mabilioni ya shilingi  hutumika katika kusambaza umeme Vijijini, kuhakikisha wananchi  wanapata huduma za maji , ujenzi wa barabara na madaraja, halikadhalika serikali hii imekuwa ikihakikisha kwamba katika sekta za kiuchumi, wananchi wanawezeshwa kufanya shughuli zao kuanzia zile ambazo ndiyo shughuli kuu za kiuchumi katika nchi yetu  ikiwa ni pamoja na  kilimo, ufugaji, uvuvi, uchimbaji wa madini pamoja na viwanda".


Matinyi  amesema kuwa  kumekuwa na mafanikio makubwa  na yote haya yanahitaji jambo moja watanzania wafahamishwe nini kina fanyika na mafanikio ni yapi  kwa hiyo tumekuwa tukitumia Wataalamu wetu Waandishi na Wapigapicha za video pamoja na za kawaida kufika katika Halmashauri zote na kuchukua maelezo ya miradi ambayo imefanikiwa pamoja ikiwa pamojana  kutengeneza vipindi vitakavyorushwa katika televisheni mbalimbali. 

Mkuu wa Mkoa wa  Iringa Bi. Halima Dendego amesema kuwa katika kuimarisha suala la Utawala Bora kwa maana ya kutengeneza miundombinu na kuwawezesha watendaji katika ofisi hizi, "Mkoa wetu ulipokea jumla ya shilingi za kitanzania Bilioni 12.524 katika kuimarisha majengo mbalimbali na pia kutoa fursa na kuwajengea uwezo wale ambao wanahudumu katika ofisi hizo".

Dendego ameongeza kwa kusema kuwa katika maendeleo ya uchumi, Mkoa wetu kwa sasa pato letu la Mkoa ni shilingi Bilioni 4.631, huku  pato la mwananchi mmoja mmoja limefikia shilingi milioni 4, 448,554, 
haya ni mafanikio makubwa kwa mwananchi mmoja mmoja, wastani huu unawafanya wananchi wa Mkoa wa Iringa kuwa ni Mkoa wa pili kutoka mkoa wa Dar es Salaam".

"Mkoa wetu umeendelea na kazi kubwa ya kukusanya mapato, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA ) imeendelea kufanya kazi nzuri sana na katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya sita, TRA imeweza kufanya kazi kwa wastani wa asilimia 95 kwa yale malengo ambayo Serikali imewapangia.

Dendego ameongeza kwa kusema kuwa  malengo ya ndani ya Halmashauri wamekuwa wakiongeza wigo na malengo ya ukusanyaji wa mapato mwaka hadi mwaka huku amebainisha kwa kusema kuwa  walianza na shilingi bilioni 24 kwa mwaka tukaja 26, na sasa tuko 29.

Aidha Dendego amesema kuwa  Halmashauri za  Mkoa wa Iringa zimeendelea kufanya vizuri na wastani wao
wa utendaji kazi ni zaidi ya asilimia 101 kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani hali ambayo inazifanya halmashauri kuendelea kutoa huduma nzuri kwa wananchi wake

"Mkoa wetu wa Iringa umeendelea kupokea fedha nyingi, katika kipindi cha miaka mitatu tumepokea wastani wa shilingi za kitanzania Bilioni 240  kwa kila mwaka
 kwa ajili ya shughuli za utawala  na shughuli za miradi ya maendeleo.

"Aidha Mkoa wa Iringa  umejikita katika kuwajengea uwezo wananchi, tumekuwa tukitoa mikopo kupitia Halmashauri zetu, na kuwa tumetekeleza agizo la serikali la kima mwaka kwa asilimia 100 na mpaka sasa tumefikia mikopo ya shilingi bilioni 7.1 kutokana na mapato ya ndani.

 "Tunasimamia ukusanyaji wa mapato hayo na kuhakikisha kwamba wale waliopata na wengine wanaendelea kupata, lakini tumewezesha kaya maskini zaidi ya elfu 30, tangia kipindi hicho tupo kwenye TASAF tatu kipindi cha pili na zaidi ya shilingi bilioni 8 zimetumika kwa ajili ya kuzifikia kaya hizi masikini" amesema RC Dendego.

Aidha ameongeza kwa kusema kuwa Mkoa wa Iringa wameweza  kutumia shilingi  Bilioni 4 .2 kwa ajili ya kufanya malipo ya moja kwa moja kwa kaya lakini Bilioni 3.2 tumetumia kutekeleza miradi 447 miradi ambayo inawajengea uwezo wale wana kaya husika ili waweze kuwa na kipato endelevu.

Amesema kuwa Mkoa wa Iringa  umeimarisha vyama vya ushirika, "tuna chama kikuu kimoja cha ushirika, lakini na vyama vidogo 54, na tumeweza kuongeza mtaji kutoka shilingi bilioni 11 mpaka bilioni 13, lakini pia tumewajengea uwezo washirika wetu wameweza kuweka hisa za kutosha, akiba, amana na vyama hivi vimetusaidia sana katika usambazaji wa ruzuku ya mbolea" amesema Dendego.

Wakati huohuo amesema kuwa zaidi ya Shilingi Bilioni 5 na tani elf 3 zimeweza kusambazwa kupitia AMCOS zetu ambazo ndio wanachama wa chaka chetu kikuu cha ushirika.

"Asilimia 82 ya wakazi wa Mkoa wa Iringa wanashiriki kwenye kilimo kama shughuli kuu ya kiuchumi katika pato la kaya, kwa hiyo katika kipindi hiki chote sisi tupo katika mikoa ambayo inazalisha zaidi na tumekuwa tukizalisha vya kutosha, wastani wetu katika miaka hii mitano ya uzalishaji ni karibu tani milioni 1.1" amesema Dendego. 

" Tumekuwa na wastani watani laki nne kila mwaka kama ziada kwa hiyo kwa maana ya uzalishaji wa chakula kila mwaka, sisi tumeendelea kuzalisha chakula na tumeendelea kuwahamasisha watu wetu kutumia mbolea bora, kupata huduma za wagani ili kuongeza tija, sasa hivi sisi tumejielekeza katika kuongeza tija"amesema Dendego. 


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...