Na.Vero Ignatus,Arusha


Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini ( LATRA)imesema kuwa basi lolote la abiria linalosafiri katika mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi itakapoguguliwa wamechezea Mfumo wa ufuatiliaji mwendo(Tracking system )kwa mabasi yanayosafiri usiku hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao sambamba na kufungiwa

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi mkuu wa (LATRA)CPA Habibu Juma Suluo wakati wa kufunga mafunzo kwa wahudumu 67 wa mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani kwa kushirikiana na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani katika Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA),kwamba itafikia wakati hawatatoa leseni ya usafirishaji hadi kwenye basi kuwepo na mhudumu aliyesajiliwa na LATRA


Aidha CPA Suluo alisisitiza kuwa mafunzo hayo yametolewa kwa mujibu wa Sheria ambapo kwa mujibu wa Kifungu Na 5(1)(e) cha Sheria ya Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini Sura ya 413, Mamlaka ina jukumu la Kusajili Wahudumu na Kuthibitisha Madereva wa vyombo vya moto vinavyotoa huduma za usafiri kibiashara.


Amesema kuwa Wahudumu hao ambao ni wanaume ni 5 na wanawake 62 wamejifunza masuala mbalimbali ikiwemo Sheria, Kanuni na Taratibu za (LATRA), Huduma bora kwa usalama wa abiria na mali, namna ya kukabiliana na malalamiko ya wateja, Huduma ya kwanza kwa mteja, Utunzaji wa mizigo pamoja na kutambua bidhaa hatarishi, Mfumo wa Tiketi Mtandao, Muitikio wa dharura, Uhusiano na mawasiliano, Unadhifu wa mtoa huduma pamoja na Utunzaji wa mazingira.

Mafunzo hayo pia yamewezakufanyika Jijini Dae es salaam kwa wahitimi 22 yaliyofanyika katika chuo cha Elimu ya biashara CBE lengo likiwa ni kuwasajili kwaajili watambulike kwaajili ya ajira

Akisoma risala kwa niamba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Hadney Chikukuro,ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia Uchumi na Rasilimali kwenye hafla ya ufungaji wa mafunzo kwa wahudumu wa mabasi ya masafa marefu na mijini Kanda ya Kaskazini, amewataka kufanya kazi kwa bidii, weledi na ufanisi ili kupunguza malalamiko kutoka kwa wateja wao.

“Ipo.wazi kwamba kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wateja wenu hasa katika namna mnavyowahudumia, ni matumaini yangu kwamba baada ya mafunzo haya mnaenda kubadili utendaji kazi wenu. Nendeni mkatumie lugha njema, zingatieni yote mliyofundishwa na kayatekelezeni kwa vitendo"Chikukuro.

Pia,Chikukuro ametoa wito kwa uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuendelea kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa weledi mkubwa ili kukifanya Chuo hicho kuwa mahali sahihi pa kupatia mafunzo stahiki na ametoa rai kwa Chuo hicho kuendelea kutoa mafunzo hayo mara kwa mara ili kuhakikisha wahudumu wanaendelea kutoa huduma zinazokidhi vigezo kwa abiria wao.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa udhibiti usafiri wa barabara Injinia Johansen Kahatano aliwataka wahudumu hao kujali Usalama wao wenyewe wanapokuwa kwenye mabasi,kwa kukaa kwenue kiti na kufunga mkanda na ikitokea kwamba wanakatazwa watoe taarifa LATRA ili waweze kusaidika

"Sisi wenyewe tumeshuhudua vifo vingi vya wahudumu kwenye mabasi,kwani wahudumu wengi hawakai kwenye viti baada ya mafunzo haya kaeni kwenye viti fungeni mikanda kwaajili ya usalama wenu na mkajiendeleze kwenye taaluma hii ''Kahatano

"Huu ni mwanzo mmeingia kwenye hii huduma siyo mwisho ingieni mkiwa na malengo endelevu jalini usalama wenu mkiona unakatazwa na mmiliki wa basi husika toa taarifa kwani usalama wako ni wa muhimu na wewe una haki kama walivyo watu wengine pia muwe mnatoa taarifa sahihi. "Kahatano,

Dkt Zainabu Mshana, ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ameishukuru LATRA kwa ushirikiano na ameahidi kuwa mafunzo hayo yataendelea kutolewa katika Kanda nyingine ili kuwafikia wahudumu wengi nchini kwa. Karibu.

Amewasisitiza wahitimu hao kwenda kuwa mabalozi wazuri kwa wahudumu wengine ambao hawakupata nafasi ya kuhudhuria kwenye mafunzo kwa kuwaelekeza masuala muhimu ya kuzingatia pindi wanapotekeleza majukumu yao ili kuifanya sekta ya usafiri ardhini kuwa bora.

"Ubalozi wenu ujikite kutambua kanuni na sheria, kutambua bidhaa hatarishi, Tiketi Mtandao, maadili, lugha njema hakikisheni mnatoa hudoma bora kwa wateja wenu"Dkt. Zainab

Vilevile, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) kwa kuendelea kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya usafiri ardhini ikiwa ni pamoja na kuiheshimisha kada ya wahudumu na kuifanya kuwa yenye tija kwa kuwa ni kazi kama kazi nyingine.

“Tunawapongeza kwa kuwa ninyi ni wahudumu wa kwanza kupata mafunzo haya na baada ya hapa, tutawapatia vitambulisho vitakavyoonesha kuwa mnatambuliwa na LATRA. Ninawasihi mkaoneshe utofauti mnapotekeleza majukumu yenu na sisi tutawafuatilia ili kuona utekelezaji wa yale mliyofundishwa,” ameeleza CPA Suluo

Akizungumza mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo, Bi. Fatma Ally Bakari amewashukuru wakufunzi kwa kuwafundisha kwa umahiri na wameahidi kuyatekeleza waliyofundishwa kwa vitendo huku akisema kuwa kabla ya mafunzo hayo hali haikuwa nzuri kwao kwani vitu vingi walikuwa hawavifahamu

Fatuma alisema wamefarijika kwa LATRA kuwa walezi wao,pia kutambua thamani yao pamoja na mabo mbalimbali waliojifunza ikiwemo kutambua mizigo hatarishi,nidhamu,lugha njema ,usafi na utunzaji mazingira watakwenda kuatendea kazi.



Wakwanza kushoto ni Dkt Zainabu Mshana, Ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) katikati ni Arusha Hadney Chikukuro,ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia Uchumi na Rasilimali akifuatiwa na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini ( latra) CPA Habibu Juma Suluo

Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia Uchumi na Rasilimali akimkabidhi cheti mmoja wawahitimu wa mafunzo ya siku tano ya wahudumu wa mabasi, katikati ni Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini ( latra) CPA Habibu Juma Suluo akifuatiwa na Kaimu mkuu wa chuo cha Uhasibu (IAA)Jijini Arusha Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini ( latra) CPA Habibu Juma Suluo akizungumza na wahudumu wa mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani mara baada yabkumaliza mafunzo ya wiki moja yaliyoendeshwa na Chuo cha

Kaimu Katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Chitukuro ambaye amemuwakilisha mkuu wa mkoa kama mgeni rasmi katika ufungaji wa mafunzo ya wahudumu wa mabasi yaliyofanyika katika chuo vha uhasibu Jijini Arusha

Mkuu wa chuo Cha Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)NIT Dkt. Zainab Mshana akizungumza kwenye hafla fupi ya wahitimu ya mafunzo ya wahudumu wa mabasi yaliyofanyika katika Chuo cha uhasibu (IAA) Jijini Arusha
Jahansen Kahatano Mkurugenzi wa mafunzo na Udhibiti usafiri barabarani (Latra)akifuatilia kinachoendelea katika hafla fupi ya wahitimu wa mafunzo ya wiki moja ya wahudumu wa mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani

Mmoja wa wahidumu wa mabasi yaendayo mkoani na nchi jirani akizungumza katika hafla fupi ya uhitimishaji wa mafunzo ya siku 5 yaliyofanyika katika Chuo Chuo ca Uhasibu Jijini Arusha.  


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...