Na Humphrey Shao,Michuzi TV

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara Annamringi Macha leo ameongoza zoezi la ugawaji Majiko ya Gesi 260 kwa Mama lishe wa kata 13 wa jimbo la Segerea.

Macha amekabidhi majiko hayo katika hafla ya utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho iliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Kamoli na kufanyika katika ukumbi wa Lekam uliopo Buguruni Jijini Dar es Salaam.

akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi majiko hayo Mh Bonnah amesema ameamua kutoa majiko hayo kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya Rais Samia Suluhu Hassan ya utunzaji wa Mazingira juu ya Nishati safi ya kupikia.

"Kumekuwa na Changomoto kubwa ya ukatwaji miti katika mikoa ya Morogoro na Pwani hii yote ni kutokana na Matumizi makubwa ya nishati ya mkaa katika Jiji la Dar es Salaam na watumiaji wakubwa wa mkaa ninhawa ndugu zangu Mama Lishe hivyo nimeona ni vyema sasa kuwapatia majiko haya watike kwenye mkaa waje kwenye Nishati safi ya kupikia" amesema Mh Bonnah.

Nae Mmoja wa Nufaika wa Majiko hayo kutoka kata ya Minazi Mirefu Mwajuma Hassan ametoa shukrani kwa mbunge huyo kwa kusema upatikanaji wa majiko hayo utasidia katika kazi zao za kila siku.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...