Mwenyekiti wa taasi ya maisha bora (ZMBF) na mke wa rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Mama Mariam Mwinyi ameishauri wizara ya afya Zanzibar kuunda kamati ya lishe ya taifa ili kukabiliana na tatizo la utapiamlo.
Mama Mwinyi ameongea hayo katika mkutano wa wadau wa lishe ulioandaliwa na taasisi ya maisha bora foundation – ZMBF inayotekeleza mradi wa lishe.
ZMBF Imetoa vitendea kazi mbalimbali kwa wahudumu TISINI wa afya ngazi ya jamii wa visiwa vya PEMBA na UNGUJA ili wawafikie wananchi kwa urahisi na kukabiliana na tatizo la lishe.
Imebainishwa katika mkutano huo kuwa upungufu wa damu unaosababishwa na lishe duni ni chanzo vya vifo vya mama na mtoto visiwani Zanzibar, imebainishwa
Mkurugenzi wa kinga na elimu ya afya wa wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Salim Slim, amesema tathmini iliyofanywa na Wizara hiyo imebaini asilimia 65.9 ya wanawake na watoto Zanzibar wana tatizo la lishe duni na upungufu wa damu hali inayo sababisha vifo vya uzazi.
Mradi wa lishe unaotekelezwa kwa ushirikiano wa ZMBF, taasisi ya BENJAMIN MKAPA - MBF na wadau wa lishe umeendelea kuhamasisha lishe bora kwa kutoa elimu kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na tayari imewafikia zaidi ya wananchi 26,000 visiwani Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...