Siku moja mara baada ya Shirika la Utangazaji Tanzania kuonyesha habari ya Mtoto Baltazari Mkina mkazi wa kijiji cha Mtoni kata ya Nakatunguru wilaya ya Ukerewe mkoa wa Mwanza akimuomba Rais Samia Suluhu Hassan amsaidie ili aweze kupata huduma za matibabu, Waziri wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu amemuelekeza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kufanya mawasiliano ya haraka na Uongozi wa Wilaya ya Ukerewe ili kumpata mtoto Baltazari kwa ajili ya kupelekwa kwenye matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando.
Waziri Ummy ameelekeza mtoto Baltazari atibiwe bure bila malipo yeyote hivyo Serikali itagharamia matibabu yake mpaka kupona kwake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...