*Ni
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF
*Ahahidi
ushirikiano, kulipa Pensheni kwa wakati,ukamilifu na usahihi
Na
Mwandishi Wetu, Dodoma
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu; Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mha. Cyprian
Luhemeja amezitaka taasisi zote zilizo chini ya ofisi hiyo kuhakikisha zinatoa
elimu juu ya kazi wanazofanya ili Wananchi waweze kuelewa majukumu yao vyema
kwa la kupatiwa huduma.
“Elimu juu ya taasisi zetu zote itolewe, haswa elimu ya Hifadhi ya Jamii iende kwa nguvu kwa wadau, naamini elimu ya Hifadhi ya Jamii ikieleweka vyema watu wengi hawatapoteza muda kwenye uwekezaji usio na tija” alisema Mha. Luhemeja.
Akimkaribisha
Bw. Badru, Mha. Luhemeja alisema, “Ndugu zangu naomba muungane nami
kumkaribisha Bw. Badru ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuongoza PSSSF, naomba
tumpatie ushirikiano ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake, Bw. Badru hii
ndio timu yako sasa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, karibuni sana”.
Mha.
Lumemeja alifurahiswa na kauli ya Bw. Badru kuwa mwelekeo wa utendaji lazima
uendane na kusudio na lengo la uwepo wa taasisi husika.
“Kweli
nimefurahishwa na hoja ya Bw. Badru, kwamba ili utendaji kazi uende vyema ni
lazima mwelekeo ulenge kusudio na lengo la taasisi husika, hivyo kila mmoja
wetu ni lazima ajue mwelekeo wa taasisi yake ili aweze kufikia malengo”
alifafanua Mha. Luhemeja.
Kwa upande wake, Bw. Badru alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumwamini na kumteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF,ameahidi utendaji bora kwa kuzingatia miongozo na kanuni zilizopo.
“Kwa
kweli nashukuru kwa kuwa sehemu ya timu hii chini ya ofisi ya Waziri Mkuu,
ninahidi ushirikiano kwenu ili kwa pamoja tuweze kutekeleza vyema majumu yetu”
alisema Bw. Badru.
Bw.
Badru alisema, PSSSF imejipanga kutekeleza vyema majukumu yake na kuendelea
kutoa huduma bora kwa Wanachama kwa kuendelea kutumia TEHAMA ili kila mwanachama
afikiwe kwa wakati.
“Tutaendelea
kutoa elimu mahususi kwa Wanachama ili waelewe zaidi juu ya PSSSF,
tunahakikisha kila mdau atafikiwa na tunaahidi kulipa pensheni kwa wakati,
ukamilifu na usahihi” aliahidi Bw. Badru
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Februari 6, 2024 alimteua Bw. Badru kuwa Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...