SERIKALI imewahakikishia kuboresha zaidi mazingira ya usalama kwa Wawekezaji na kuendelea kuwapa ushirikiano ili kusaidia Serikali kutoa ajira za kudumu na za muda mfupi kwa wazawa .

Akizungumza na Wanahabari Leo Februari 20,2024 Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam  Omary Kumbilamoto wakati akifungua tawi  jipya la duka la viatu la Kampuni ya Relaxo Amesema Serikali peke yake haiwezi kutoa Ajira kwa Vijana wote nchini hivyo panapotokea wawekezaji wengi inaleta faraja na mtazamo mzuri kuhakikisha Vijana wanaendelea kutafuta vipato vyao kupitia wawekezaji wenye dhamira ya dhati ya Kumsaidia Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan  kuhakikisha zinapatikana fursa za ajira na viwanda vingi nchini.

Hata hivyo Meya amesema kuendelea kuwepo kwa wawekezaji hao nchini ni ishara tosha kuwa usalama upo na umeimarishwa na Kamanda  Jumanne Murilo katika kuhakikisha analisimamia hilo kwa asilimia zote kwa Wawekezaji nchini

Aidha amewapongeza pia Kampuni hiyo kwa kuweka muda sahihi wa kuuza bidhaa hizo kwa muda wa usiku ili kuwapa nafasi watu wengi kufika katika maduka yao na kupata huduma .

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Best brands  kupitia Khalid Mohammed Salim amesema Kampuni imejipanga kuwafikia wateja wake kwa maeneo ya karibu na Jiji ambapo leo Tawi jipya la Relaxo mitaa ya Samora  litakwenda kugawa ajira kwa vijana zaidi ya 50 huku dhamira yao ya dhati ifikapo 2025 nchini Tanzania kupitia Jiji la Dar es Salaam .

"Kipekee tumepata maombi mengi ukizingatia viatu vyetu tumelenga zaidi upande wa kimichezo hivyo wanamichezo wengi wanapenda kupata viatu vyenye ubora zaidi ndio maana tukawiwa kuendelea kufungua matawi katikati ya mji hili la leo tumezindua ni la tatu na tuna mpango wa kufungua  maduka 20 sanjari na ujenzi wa Kiwanda cha uzalishaji wa viatu hivyo ili kuwafikia wateja wao kwa haraka kutokana na ubora wa viatu hivyo."

Aidha Salim ameongeza kuwa viatu vyao vinayozalishwa vimesheheni viatu kwa rika zote na sehemu mbalimbali eza mahususi ikiwemo kwa matumizi ya mashuleni,hospitalini na sehemu zingine zenye matumizi ya viatu.

Pia amesema Kampuni hiyo imetoa ofa ya kuhakikisha watakaohitaji kuuza bidhaa hizo watagharamiwa fremu za biashara ili kuendelea kuzitangaza bidhaa hizo.

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akiwa na Mkurugenzi wa wakala wa bidhaa za Viatu (Best brands) Khalid Mohammed Salim kulia kwake wakati kushoto kwake mwanafamilia wa best brands Salim Kikeke pamoja na Msanii wa Vichekesho chekeshaji nchini Mpoki Leo Februari 20,2024 wakati wa kikata utepe kuashiria ufunguzi wa tawi jipya la tatu la bidhaa za viatu lilipo mtaa wa Samora Jijini Dar es Salaam

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akizungumza na Wanahabari machache mara baada ya kuzinduliwa kwa Tawi jipya la duka la viatu la Kampuni ya Best brands na Kuwahakikishia Serikali itaendelea kuwashika mkono Wawekezaji nchini na ili kuendelea kuisaidia Serikali kutoa ajira kwa wingi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...