Na Issa Mwadangala
Mkuu wa Mkoa wa Songwe ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Mkoa Dkt. FRANSIS MICHAEL amempongeza Kamanda wa Polisi Mkoani humo kwa kupandishwa cheo hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akitoa Pongezi hizo leo tarehe 26 Februari 2024, alipotembelewa na Kamanda Mallya huko ofisini kwake Dkt. FRANSIS amebainisha kuwa, kitendo cha Kamanda huyo kupandishwa cheo na Mheshimiwa Rais ni kuaminiwa na kuonesha utendaji kazi mzuri ndani ya Mkoa huo ambao ni lango la SADC.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe ambaye amepandishwa cheo kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) THEOPISTA MALLYA pamoja na kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa kumpandisha hicho, ameahidi kuwa ataendelea kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ili Mkoa huo uendelee kuwa shwari wakati wote.
Pia amemshukuru Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Mkoa wa Songwe kwa usimamizi wao mzuri katika utendaji wa kazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...