JESHI la Polisi mkoa wa Mwanza linawashikilia watu wawili ambao ni Sophia James (42), mkazi wa Buswelu, wilaya ya Ilemela na Kulwa Kapuli, (42), fundi ujenzi na mkazi wa Buswelu kwa tuhuma za kuendesha shughuli za upasuaji wa mawe kwa kutumia baruti bila kuwa na kibari na kusababisha majeraha kwa watu wawili kwa kujeruhiwa na mawe yaliyowapiga wakati wanapita karibu na eneo ambalo shughuli ya ulipuaji wa mawe hayo ilikuwa ikiendelea.

Tukio hilo limetokea tarehe 17, 02.2024 muda wa saa 16:00 jioni katika eneo la Magaka, kata ya Kahama, wilaya ya Ilemela ambapo Arson Philipo (9), mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Kahama na Dunia Elisha (12), mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Kahama, walijeruhiwa na mawe sehemu mbalimbali za miili yao wakati wanapita karibu na eneo hilo.

Majeruhi hao ambao ni Arson Philipo aliyejejuhiwa kwa kukatwa na vipande vya mawe mguu wa kulia karibu na unyayo pamoja na shavu la upande wa kulia, alipelekwa katika Hospitali ya Sekou-Toule na Dunia Elisha alijeruhiwa mkono wa kulia, usoni upande wa jicho la kushoto na puani naye amelezwa katika Hospitali ya Bugando. Wote wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri. Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linawataka wakazi wa Mwanza hususani wanaofanya shughuli za ulipuaji wa Mawe kufuata sheria pamoja na kuchukua tahadhari zote wakati wakuendesha zoezi la ulipuaji wa Mawe sehemu za makazi ya watu ili kuepuka madhara kwa watu na mali kuathiriwa kutokana na mlipuko wa mawe.

Katika tukio jingine, tarehe 17,02.2024 muda wa saa 14:00 mchana huko mtaa wa Ihila “B”, kata ya Buhongwa nyumba ya vyumba vitatu mali ya Jaribu Nyamonge (48), mkazi wa Dar es Salaam iliteketea kwa moto na kusababisha kifo kwa mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi sita aitwaye Thomas Alex aliyekuwa na wenzake wawili ndani ya nyumba hiyo.

Aidha, katika tukio hilo watoto wengine wawili wa familia hiyo waliokolewa kwa jitihada za wananchi, Jeshi la zima moto na uokoajai pamoja na Jeshi la Polisi ambapo mama wa watoto hao aitwaye Jenipher Richard (24), mfanyabiashara na mkazi wa mtaa wa Ihila hakuwepo alikuwa kwenye biashara yake.

Moto huo uliweza kudhibitiwa kutokana na juhudi za wanachi, Jeshi la zima moto na uokoaji pamoja na Jeshi la Polisi, Chanzo cha moto huo kinachunguzwa na mwili wa Thomas Alex umehifadhiwa katika Hospitali ya Bugando kwa uchunguzi.

Tunawaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kuendelea kufichua matukio ya kihalifu katika jamii ili tuweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wote watakao bainika kupanga, kujaribu na kufanya uhalifu kwa njia yoyote ile kwa kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Pia, kuchukua tahadhari za kiusalama kwa watoto ili kuwaepusha na matatizo yanayoweza kuwapata kwa kukosa usimamizi.

Imetolewa na: -

Wilbrod W. Mutafugwa - DCP
Kamanda wa Polisi

Mkoa wa Mwanza

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...