Na Albano Midelo,Songea

JAJI Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Songea Mheshimiwa James
Karayemaha amesema mifumo ya utoaji na upatinaji haki nchini ni muhimu
kuboreshwa na kuimarishwa ili iweze kuleta usawa na ustawi katika jamii.

Jaji Karayemaha amesema hayo wakati anazungumza kwenye kilele cha
maadhimisho ya siku ya sheria nchini ambazo kimkoa zimefanyika kwenye
viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Songea.

Amebainisha kuwa utoaji na upatikanaji wa haki utawezekana ikiwa
kutakuwa na mifumo imara na jumuishi baina ya Taasisi hususan kwenye
eneo la vitendea kazi vya kisasa vya TEHAMA na uwepo wa miundombinu
wezeshi baina ya Taasisi ya haki jinai.

“Mahakama imekuwa ikifanya maboresho kwenye huduma zake ili kutoa
huduma bora inayomlenga mwananchi kupitia Mpango Mkakati wa miaka
mitano ambao umesimikwa katika nguzo tatu zinazoongoza katika
utekelezaji na Programu za kimaboresho’’,alisisitiza Jaji Mfawidhi.

Amezitaja nguzo hizo kuwa ni mahakama kutekeleza utawala
bora,uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali,upatikanaji na utoaji wa haki
kwa wakati na kuthamini imani kutoka kwa wananchi,watumiaji wa
huduma za mahakama na jamii kwa ujumla.

Akizungumzia umuhimu wa mfumo jumuishi Jaji Mfawidhi huyo Mahakama
Kuu Kanda ya Songea,amesisitiza kuwa kuanzishwa kwa Mfumo Jumuishi
wa Taasisi za Haki Jinai utasaidia upatikanaji wa taarifa kwa wakati
muafaka,kuondoa urasimu na utendaji kazi katika hatua mbalimbali zilizopo
kwenye Taasisi za Haki Jinai hivyo haki kutolewa kwa wakati.

Hata hivyo amesema TEHAMA ina nafasi kubwa katika kuboresha haki
na kufanikisha upatikanaji wa haki kwa wakati ambapo amesema
Mahakama inaendelea kuboresha huduma zake kupitia mifumo ya
TEHAMA.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas
akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho hayo ameipongeza Idara ya
Mahakama Kuu Kanda ya Songea kwa kupiga hatua kubwa katika utoaji
haki hasa baada ya kuboresha miundombonu ya mahakama ikiwa ni
Pamoja na matumizi ya TEHAMA.


RC Thomas ameipongeza Mahakama Kuu Kanda ya Songea kwa kutatua
changamoto ya mlundikano wa mashauri ambapo hivi sasa mashauri
yenye muda mrefu yamebakia machache.

Ameipongeza Mahakama hiyo kwa kupeleka vifaa vya TEHAMA katika
magereza ya Tunduru na Mbinga ambavyo vinakwenda kutumika kwa ajili
mfumo wa jumuishi wa haki jinai kwa ajili ya kusikiliza mashauri kwa njia ya
mtandao.

Amesisitiza kuwa juhudi zinazofanywa na vyombo vyote vya haki jinai zina
mchango mkubwa kwa jamii ambapo ameshauri kushirikiana ili
kuunganisha mifumo ya utendaji kazi hatimaye kufikia mafanikio makubwa
katika utoaji haki.

Kaulimbiu ya mwaka huu kwenye maadhimisho ya siku ya sheria nchini
inasema umuhimu wa dhana ya haki kwa ustawi wa Taifa;nafasi ya
mahakama na wadau katika kuboresha mfumo jumuishi na haki jinai.


Jajji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Songea Mheshimiwa James Karayemaha ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini ,maadhimisho ambayo kimkoa yamefanyika kwenye viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Songea.

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini.
Baadhi ya mahakimu wa Kanda ya Songea wakiwa kwenye maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...