Wakazi wa Kata ya Lukobe Manispaa  ya Morogoro wameiomba Serikali kuona namna ya kuwasaidia, kuwahamisha wananchi  waliyopo kwenye mkondo wa daraja la mradi wa SGR,   kuondokana na adha ya mafuriko ambayo katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikijitokeza kila mwaka 


Wameyasema hayo mbele ya Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mhe. Abdulaziz M. Abood alipofika kutoa pole kwa waadhilika wa Mafuriko katika Kata za  Lukobe na Kihonda ambapo alifika mtaa wa  Azimio eneo lenye waathilika wengi. 

Wakazi hao walipata nafasi  kuzungumza na kutoa maoni pamoja na kero  mbele ya Mbunge  ambapo wamesema awali kabla ya Mradi wa reli ya  Mwendo kasi maeneo hayo hayakuwahi kupata mafuriko tofauti na sasa baada ya kujengwa tuta ambalo linazuia maji kupita kwenye  njia yake na kurudi kwa wananchi

Rashidi Kibwana  mmoja wa wakazi wa Azimio pamoja na kuiomba Serikali kuwatatulia changamoto  inayowakabili pia ameishukuru Serikali ya Mhe Rais Samia kwa namna ambavyo imekuwa  karibu sana na wananchi wake pale wanapopatwa na changamoto.

 Pia amemshukuru Mbunge Mhe Abood kwa namna ambavyo kila wakati bila kujali muda wala nyakati amekuwa kimbilio na sikio la wananchi katika Jimbo lake la Morogoro  Mjini.

'Mimi nimeishi Morogoro  sasa zaidi ya miaka  48  lakini sijawahi kuona Mbunge anayependa wananchi na kuwasaidia bila kuchoka kama alivyo Mhe Abood" Alisema Rashidi
 
 Baada ya kusikiliza kero hizo ikamlazimu kuwaitwa wataalamu wanaosimamia na kujenda mradi wa SGR kwa Morogoro, na baada ya kufika watalaamu wanaosimamia mradi uwo ndipo 

Baada ya kusikiliza kero na maoni ya wananchin Mhe Abood ametaka kuwa watulivu wakati Serikali  ikitafakari namna ya kuwasidia na kuwahakikishia wakazi wa Kata za Lukobe na Kihonda kuwa kilio chao Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekisikia na anakutfutia ufumbuzi.

Pia Mhe Abood akawaomba wasimamizi wa amradi wa SGR  kutumia  athari za mvua kuangalia kwa namna gani wataweza kuzuia maji yasiingie kwenye makazi ya watu


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...