HAKAMA Kuu ya Mkoa wa Iringa chini ya Jaji Mfawidhi Mgetta leo Februari 1, 2024 imesikiliza kesi ya Rufaa Namba 84101/2023 kati ya Maria Ngoda dhidi ya Jamuhuri.
Akiongoza jopo la Mawakili upande wa mkata rufaa Wakili Moses Ambwindile amesema leo wametetea sababu zao za Rufaa 14 mbele ya Jaji Mfawidhi.
Aidha Jaji Mgetta ameahirisha shauri hilo mpaka hapo kesho tarehe 2 Februari 2024.
Mfungwa Maria Ngoda (mkata rufaa) alihukumiwa kifungo cha miaka 22 kwa kukutwa na vipande 12 vya nyama ya swala Novemba 3,2023.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...