Kikos cha Timu ya Tabora United leo kimeanza maandalizi kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya NBC Soka Tanzania Bara ambapo itamkaribisha Azam FC Februali 19 mwaka huu katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi hapa Mjini Tabora.

Kikosi hicho cha nyuki wa Tabora kimeanza mazoezi ikiwa ni mara baada ya kutoka kumaliza mzunguko wa kwanza hapo jana dhidi ya Namungo na kutoka sare ya goli moja kwa moja lililofungwa na Erick Okutu.

Tabora United chini ya kocha Mkuu ,Goran Copnovic inaendelea kujifua ili kujiweka vizuri kwenye michezo ya mzunguko huo wa pili wa Ligi kuu ya NBC Tanzania Bara pamoja na michuano ya kombe la Azam Sport Federation ASFC.

"Tumemaliza mzunguko wa kwanza jana na Namungo na sasa tunajiandaa na mzunguko wa pili ambapo tutakutana na Azam FC Februali 19, na hali ya kikosi iko vizuri hivyo tunazidi kujipanga.

Mzunguko wa kwanza umemalizika tukiwa na jumla ya alama 16, hatuko vizuri kimahesabu kulingana na malengo ambayo tulikuwa tumejiwekea kama Timu, lakini bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye michezo iliyopo mbele yetu.

Aidha kwa upande wa Afya za wachezaji ,kuna majeruhi wawili ambao ni Kevin Pemba Kingu na Erick Okutu mfungaji wa goli la jana dhidi ya Namungo ambaye alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kuumia huku Kipa namba moja John Noble akisumbuliwa na Malaria.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...