NAIBU  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amewataka wadau wa Sekta Mtambuka kuongeza nguvu zaidi katika kupata fedha na kushirikiana na Serikali katika kufanikisha masuala anuai yahusuyo huduma ya maji kwa Watanzania.

Amesema hayo wakati akifunga Mkutano wa sita wa Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji Jijini Dar es Salaam.

Amesisitiza umuhimu wa kuongeza wadau wa Jukwaa ili kuyafikia makundi mengi katika jamii pia kuongeza nguvu ya ushirikishwaji.

Ameongeza  ni muhimu kuwa nabmipango inayotekelezeka ya kufanikisha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa masuala mbalimbali yaliyokubalika na jamii.

Mkutano wa sita wa Jukwaa la Kitaifa la Wadau wa Sekta Mtambuka katika usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za maji umefanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam likiwa limebeba kaulimbiu  isemayo; Majanga ya Mafuriko na Ukame:  Uwekezaji katika Usalama wa Maji ni Jambo la Haraka.

Mhandisi Mwajuma ni mmoja kati ya vinara wanawake katika masuala ya uhandisi na huduma kwa jamii hapa nchini.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...