Katika kudumisha jitihada za Serikali kwenye kampeni ya matumizi safi na salama ya gesi za majumbani, Umoja wa Wafanyabiashara wa Gesi (LPG) za Mitungi ya Majumbani nchini (TZLPGA) wamekutana na waandishi wa habari kujadili njia endelevu za kukuza sekta hio kupitia uwezeshaji wa taarifa.

Umoja huo ulioanzishwa mwaka 2023 unaundwa na kampuni 6 zinazofanya biashara ya gesi za mitungi kwa matumizi ya majumbani ambazo ni CAMGAS, O-GAS, LAKE GAS, TAIFA GAS, ORYX GAS, MANJI GAS na PUMA ENERGY.

Akizungumza na waandishi wa habari waliohudhuria mjadala huo, Mkurugenzi Mkuu wa umoja huo, Amos Jackson alinukuliwa, ‘tunaamini kuwa ukusanyaji na usambazaji wa taarifa sahihi kwenye sekta hii utasaidi kuleta mageuzi makubwa kwenye kufanikisha azma ya nchi yetu kupiga hatua kwenye matumizi ya gesi za mitungi majumbani. Kwaio uwepo wenu hapa utasaidia sana kupanua ufahamu wetu kupitia maoni yenu kama wadau muhimu wa sekta hii’.

Amos alinukuliwa kuhusu mikakati iliyowekwa na umoja huo, alisema, ‘tumedhamiria kupanua matumizi ya teknolojia hii ya gesi za majumbani katika katika kupunguza uzalishaji wa kaboni, kuboresha ufanisi wa nishati, na kurahisisha matumizi mbadala za nishati safi’.

Aidha, Mwenyekiti wa TZLPGA Benoit Araman alisisita kuhusu umuhimu wa kudumisha ushirikiano baina ya wadau wa sekta hio na serikali. Alisema, ‘ni wajibu wetu kuiunga mkono serikali kuhakikisha tunaleta mapinduzi kwenye sekta hii ya gesi majumbani ili kutokomeza uharibifu wa mazingira unatokokana na matumizi ya mkaa’. Aliendelea, ‘mkaa ni tishio kwa maana huchangia kutengeneza hewa ya kaboni ambayo inachafua mazingira na kuleta mabadiliko hasi ya tabia ya nchi’. 

Mdhahalo huo uliohudhuriwa na mgeni rasmi, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dr. James Andilile ambae ameunga mkono uzinduzi wa kampeni wa kusambaza taarifa sahihi juu ya matumizi salama ya gesi (LPG) kwa manufaa ya taifa kwa ujumla.

TZLPGA imeahidi kushirikiana na wadau wa sekta hio kutoa msukumo wa wawekezaji kutoa pesa kwa ajili ya kukuza matumizi ya nishati safi na athari zingine chanya zitakazosaidia kuwa tija kwa sekta ya nishati kwa ajili ya maendeleo ya Taifa zima.

Mkurugenzi Mkuu wa TZLPGA, Amos Jackson akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye mjadala huo

Mwenyekiti wa TZLPGA, Benoit Araman akizungumza na wageni waalikwa kwenye mjadala huo (hawapo pichani


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...