Watalaam wa upasuaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na wenzao kutoka nchini Marekani wamekamilisha kambi maalum ya siku tano iliyohusisha upasuaji wa urembo na upasuaji wa matibabu (Cosmetic and Reconstructive Surgery) kwa wagonjwa nane.Akizungumza wakati wa kuhitimisha kambi hiyo na kwa niaba ya timu nzima iliyoshiriki, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa MNH, Dkt. Ibrahim Mkoma, amesema upasuaji uliofanyika ni wa matibabu kwa wagonjwa waliokuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo waliopata ajali ya kuungua moto na wenye misuli iliyokakamaa kutokana na majeraha n.k.

Amesema, kuna mtoto ambaye kichwa chake kilizaliwa kikiwa na vinundu vidogo vidogo mithili ya visunzua (skin tag) ambavyo viliondolewa na kufanya sehemu kubwa ya kichwa chake kuwa na kipara, hivyo amefanyiwa upasuaji wa kuwekewa puto (tissue expander) kwenye kichwa sehemu yenye nywele karibu na kipara ili ngozi ya eneo hilo iweze kuongezeka na kukuza nywele ambazo baada ya mwezi mmoja  zitakuwa zimeota sehemu kubwa na kuruhusu kufanyiwa upasuaji wa kuvuta ngozi hiyo ikiwa na nywele na kufunika sehemu yenye kipara hivyo kumwezesha mtoto huyo kurudi katika hali yake ya kawaida.

Upasuaji huo umefanyika kwa kushirikiana na Watalaam wa Upasuaji kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la Marekani ReSurge International ambao wana uzoefu mkubwa duniani katika kujenga uwezo wa kufanya upasuaji wa matibabu na urembo.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...