Na Said Mwishehe, Michuzi TV- Tabora
WAZIRI
wa Kilimo Hussein Bashe amezindua Ofisi za Benki ya Meandeleo ya
Kilimo(TADB) Kanda ya Magharibi huku akitumia nafasi hiyo kueleza
umefika wakati wa kuwa na sera ya fedha katika kilimo lengo likiwa
kuwawezesha wakulima kupata mikopo yenye riba nafuu tofauti na
ilivyosasa ambapo wanakopa katika benki zenye mlengo wa kibiashara.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa ofisi za Benki ya TADB Kanda ya Magharibi Mjini
Tabora , Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kanda hiyo inajumuisha
Mkoa wa Tabora, Kigoma na Katavi na uwepo wa ofisi za benki hiyo katika
kanda hiyo inakwenda kusogeza huduma karibu na wakulima.
Akielezea
zaidi kuhusu mikakati ya Serikali katika kilimo amesema pamoja na mambo
mengine iko haja ya kuwa na sera ya fedha itakayohusu sekta ya kilimo
ambayo itatoa fursa ya wakulima kuwa na uwezo wa kukopesheka kwa urahisi
na bila ya kuwepo kwa vikwazo ambavyo vinasababishwa na kutokuwepo kwa
sera ya fedha katika kilimo.
"Jambo la pili ambalo nataka niseme
na kwa kuwa mwakilishi wa Benki Kuu ya Tanzania(BoT) yuko hapa , mikopo
katika sekta ya uchumi wa nchi yetu uchumi wote mikopo inayoingia ni
zaidi ya Sh.trilioni 20 na inayokwenda sekta ya kilimo ni asilimia chini
ya 10...
"Na bado ukienda kwenye uzalishaji katika kilimo fedha
inayotolewa kama mkopo ni ndogo sana.Sasa hoja yangu na nimeshaongea na
Waziri wa Fedha , Gavana wa Benki Kuu , Waziri wa Mipango na
ninawaandikia barua.
"Tunahitaji sera ya fedha ya kilimo kwani
haiwezekani kilimo kikopeshwe kwa kutumia sera za benki za
biashara.Kutumia sera hiyo bado hatutoweza kutoa watu kwenye umasikini,"
amesema Waziri Bashe.
Ameongeza Rais Dk.Samia Suluhu Hassan
anafanya jitihada kubwa katika kuinua sekta ya kilimo na kuboresha
maisha ya wakulima akitolea mfano ujenzi wa miundombinu ikiwemo ya
kilimo cha umwagiliaji unaofanywa na Serikali.
"Serikali
ikashamaliza kuboresha miundombinu mkulima anahitaji fedha ya kununua
mbolea , pembejeo na mambo mengine yanayohusu kilimo.Kwa hiyo ni muhimu
tukawa na sera ya kupata mitaji kwenye sekta za uzalishaji kilimo,
mifugo na uvuvi."
Amesisitiza lazima kuwe na sera inayoeleweka na
yeye kama Waziri wa Kilimo atawasukuma wote wanaohusika ili kupata
sera hiyo na anaamini itafanikiwa.
Amefafanua katika kipindi
kisichozidi miaka miwili Rais Samia ameipatia TADB Sh.Bilioni 632."Sasa
ni sheria zipi zinazoisimamia TADB kukopesha ?Kwa sasa ni kama benki
za biashara.Hatuwezi, kwa hiyo lazima tutoe maamuzi na nimuombe Gavana ,
Waziri wa Fedha amenielewa, Waziri wa Mipango amenielewa tufanikishe
jambo hili.
"Tutahakikisha tunasukuma tuwe na sera ya fedha
katika sekta ya kilimo katika nchi hii ili tuweze kufika mahali ambako
tunatakiwa kwenda, " amesema Waziri Bashe huku akitumia nafasi hiyo
kuagiza jengo la ofisi za TADB kupewa jina la aliyekuwa Mwenyekiti wa
CCM Mkoa wa Tabora Hassan Mwakasuvi aliyefariki dunia juzi na lengo la
ofisi kupewa jina lake ni kuenzi mchango wake mkubwa katika kilimo ndani
na nje ya Mkoa wa Tabora.
Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya
Maendeleo ya Kilimo(TADB) Frank Nyabundege amekieleza umuhinu wa ofisi
ya TADB Kanda ya Magharibi amesema toka mwaka 2018, mikoa ya Kigoma,
Katavi na Tabora ilikuwa ikihudumiwa na ofisi ndogo iliyokuwa Kigoma na
baadae kuhamishiwa Tabora.
Ameongeza kwamba hadi kufikia
Februari, 2024, TADB imekwisha wezesha wakulima na wafugaji kwa kutoa
mikopo yenye jumla ya thamani ya Sh.bilioni 19.59 (Mkoa wa Kigoma, Sh.
bilioni 7.209, Mkoa wa Katavi, Sh. bilioni 2.394, na Mkoa wa Tabora,
Sh.bilioni 9.996).
"Mikopo hii imetolewa kwenye miradi ya mpunga,
chikichi, maharage, mahindi, unenepeshaji wa ng’ombe, tangawizi,
ufugaji wa kuku, ufugaji wa nguruwe, na ufugaji wa kondoo. Benki
inaendelea kuweka mikakati thabiti ya kukopesha kwenye zao la tumbaku,
pamba na asali, kwani mazao haya yanachangia kukuza uchumi wa mkoa wa
Tabora."
Aidha ameishukuru Ofisi ya Manispaa ya Tabora, kwa
kutupatia jengo hilo la ofisi kwa miaka 33 bure. Hiyo ni ishara kubwa ya
ushirikiano kati ya Mkoa wa Tabora na benki yao, hivyo ameahidi jengo
hilo kutumika vizuri.
Ameongeza wanatamani kuendelea kusogeza
huduma kwa wananchi na endapo ikimpendeza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kutoa
jengo Kigoma Mjini bure, anaahidi benki hiyo iko tayari kufungua ofisi
ndani ya mwaka huu wa 2024.
Waziri wa Kilimo Husen Bashe akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kilimo nchini(TADB)Frank Nyabundege mara baada ya kuwasili wakati wauzinduzi wa Tawi la benki hiyo mkoani Tabora
Waziri wa Kilimo Husen Bashe akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kilimo nchini(TADB)Frank Nyabundege mara baada ya kuwasili wakati wauzinduzi wa Tawi la benki hiyo mkoani Tabora
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo(TADB) akomuonesha ramani ya mikoa na wilaya ambayo benki hiyo ipo nchini Waziri wa Kilimo Hussen Bashe wakati wa uzinduzi wa tawi la benki yiyo mkoani Tabora.
Waziri wa Kilimo Hussen Bashe akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tawi la Benki ya TADB Kanda ya Magharibi inayojumuisha Mkoa wa Kigoma, Tabora na Katavi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...