Katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji katika sekta ya Elimu, tarehe 22 Machi 2024, Mhe. Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Msumbiji alikutana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Joaquim Chissano, Prof. José Magode kwenye Ofisi za Chuo hicho zilizopo Jijini Maputo.

Katika Mkutano huo, pamoja na masuala mengine ya ushirikiano, Viongozi hao wawili walikubaliana kuanzishwa Darasa la Lugha ya Kiswahili Chuoni hapo ambapo Ubalozi uliahidi kusaidia kupatikana kwa Walimu watakaofundisha Darasa hilo.

Imetolewa na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Maputo.
22 Machi, 2024
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...