BARAZA la Sanaa, Sensa, Filamu na Utamaduni la Zanzibar, (BASSFU)limemfungia msaanii wa kizazi kipya Zuhura Othman Masoud maarufu Zuchu kuendesha shughuli zote za sanaa visiwani Zanzibar.

Akizungumza leo Machi 5, 2024 ofisini kwake na waandishi wa habari, katibu mtendaji wa baraza hilo, Omar Abdalla Adam amesema baraza limemfungia kwa kipindi cha miezi sita kuanzia sasa pia imepiga marufuku redio na televisheni za Zanzibar kupiga nyimbo zake zote kwa kipindi cha miezi sita.

“Baraza lina wajibu wa kusimamia mila, silka desturi na utamaduni wa Mzanzibari, kwa hiyo linatamka rasmi kumfungia msanii Zuhura Othman Soud (Zuchu) kufanya shughuli yoyote ya sanaa kwa Zanzibar kwa kipindi cha muda wa miezi sita kuanzia leo Machi 5, 2024."


Hatua hiyo imekuja baada ya tukio la Februari 24 mwaka huu Zuchu wakati akitumbuiza katika usiku wa Fullmoon Kendwa Mkoa wa Kaskazini Unguja kudaiwa kuimba nyimbo, kutoa matamshi na kuonyesha ishara mbaya ambazo ni kinyume na maadili ya kizanzibari.

Aidha amesema wanafanya hivyo kutokana na tabia yake kuimba nyimbo ambazo hazina maadili, hazifuati misingi na hazina afya njema kwa jamii ya Wazanzibari.

Pia, amesema licha ya msanii huyo kutokuwa na usajili Zanzibar lakini amekuwa akiendesha shughuli zake za sanaa bila kupata kibali.

Mbali na adhabu hiyo, pia msanii huyo ametakiwa kulipa faini ya Sh1 milioni moja kwa Baraza la Sanaa na aandike barua ya kuomba radhi na kuthibitisha kwamba hatafanya kosa hilo ndani ya kipindi alichofungiwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...