Na Pamela Mollel,Arusha

Katibu msaidizi ofisi ya Rais sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya kaskazini Bw. Gerald Mwaitebele amewataka Viongozi wa umma na watumishi kuzingatia maadili ili kuweza kupata viongozi wenye uadilifu.

Bw Mwaitebele ameyasema hayo alipokuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya miaka 57 toka kutangazwa kwa Azimio la Arusha yaliyofanyika katika viwanja vya makumbusho ya azimio la Arusha.

Alisema kuwa kupitia maadhmisho ya makumbusho ya azimio la Arusha viongozi wa umma watumishi na wananchi wanapaswa kuzingatia maadili ili kuwezakupatikana viongozi wenye uadilifu.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo cha makumbusho ya azimio la Arusha dkt Kamala Gwakisa alisema kuwa lengo la maadhmisho ya kumbukizi ya miaka 57 ya kuzaliwa kwa Azimio la Arusha ni kulinda uhuru wa taifa na mataifa ya jirani,kuheshimiana na kuendeleza uzalendo.

Aliongeza kuwa katika maadhmisho hayo waliweza kuzindua maonesho mapya ya makumbusho,kuzindua makala maalum ya Azimio la Arusha pamoja na maktaba.

Naye afisa maadili kutoka ofisi ya Raisi sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma bw musiba magoma amewataka wanafunzi na jamii kwa ujumla kuzingatia maadili na kuwa na uadilifu huku akiwasihi vijana wa vyuoni Kuepuka vishawishi na simu ambazo hawana uwezo nazo.

Mmoja wa mwanafunzi aliyeshiriki maadhmisho hayo Jeska valeriani alisema kuwa kupitia maadhmisho hayo amejifunza uzalendo,maadili na uwajibikaji.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...