Benki Kuu ya Tanzania ikiongozwa na Gavana Emmanuel Tutuba, imefuturisha wakazi wa jiji la Dodoma ambapo wageni mbalimbali wamehudhuria hafla hiyo wakiwemo viongozi wa serikali na dini, taasisi za fedha, makundi maalumu, vituo vya watoto yatima pamoja na wafanyakazi wa Benki Kuu.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika tarehe 26 Machi 2024 katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo, Gavana Tutuba amewasihi viongozi wa dini na wananchi wote kuliombea taifa liendelea kuwa na utulivu, mshikamano na amani ili kuwawezesha wananchi kuendelea kufanya kazi kwa ustawi na maendeleo ya taifa kwa ujumla. “Baraka tunazoendelea kuzipokea kama nchi inawezekana zinatokana na maombi ya kila mmoja wetu,” alisema.

Gavana Tutuba aliongeza kuwa katika ukanda wa Afrika Mashariki, Tanzania imekua na uchumi imara zaidi pamoja na uwepo wa changamoto mbalimbali za kiuchumi duniani.

Kwa upande wake Naibu Gavana (Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha), Bi. Sauda Kassim Msemo, alisema kuwa Benki Kuu kama ilivyo kwa taasisi nyingine nchini, huandaa hafla kama hii ya leo, kwa wafanyakazi wake, lakini pia kwa kuwaalika wadau wake mbalimbali ili kujumuika kwa pamoja na kumshukuru Mwenyezi Mungu.

Wakizungumza awali, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajab Shabani na Mchungaji John Kamoyo kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) wameipongeza Benki Kuu kwa kuandaa hafla hiyo iliyohusisha makundi mbalimbali katika jamii na kusisitiza umuhimu wa waumini wa dini zote kuendelea kushirikiana katika kujenga na kukuza uchumi wa nchi yetu.

 

Gavana Emmanuel Tutuba akifurahia jambo alipowasili katika hafla iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Naibu Gavana, Bi. Sauda Kassim Msemo, Meneja Idara ya Mawasiliano, Bi. Victoria Msina, Mkurugenzi wa Tawi la BoT Dodoma, Dkt. Wilfred Mbowe, na Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano, Bi. Noves Moses.

 

Naibu Gavana (Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha), Bi. Sauda Kassim Msemo, akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.

 

Mchungaji John Kamoyo kutoka Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.

 

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Rajab Shabani, akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.

 

Gavana, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza katika hafla ya futari iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.

 

Gavana Emmanuel Tutuba akipewa maelezo na mhudumu kuhusu aina za uji zilizopo katika hafla ya futari iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.

 

 Wageni waalikwa wakipata futari katika hafla iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.

 

Gavana Emmanuel Tutuba katika picha ya pamoja na watoto kutoka vituo vya watoto yatima vya jijini Dodoma.Wageni waalikwa wakifuatilia hotuba ya Gavana Emmanuel Tutuba wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na BoT katika Ukumbi wa Jenerali Venance Mabeyo jijini Dodoma.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...