Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Diamond Trust (DTB), Ravneet Chowdhury (kushoto), akikabidhi msaada wa kompyuta 100 zenye thamani ya Sh. milioni 35 kwa Mkurugenzi Mtendaji wa  Kituo cha Kuendeleza Elimu cha Lauren (LEPC), Felicia Felix (wa pili kushoto), Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Songoro Mnyonge, Ronadina Kimaro (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha msaada kwa Wajane na Watoto (CWCA), Utti Mwang’amba, zilizotolewa na benki hiyo, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam leo, ikiwa ni mkakati wake wa ushirikiano na jamii wa kuendeleza elimu ya TEHAMA kwenye shule za sekondari.
Afisa wa Elimu ya Watu Wazima Manispaa ya Kinondoni Explancer Siame akishukuru msaada kutoka Benki ya DTB.
Wafanyakazi wa Benki ya Diamond Trust (DTB) wakiwa wameambatana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Diamond Trust (DTB), Ravneet Chowdhury (Wa tano kutoka kulia) wakionesha baadhi ya kompyuta zilizotolewa kwa Kituo cha Kuendeleza Elimu cha Lauren (LEPC), Shule ya Sekondari ya Songoro Mnyonge, na Kituo cha msaada kwa Wajane na Watoto (CWCA), zilizotolewa na benki hiyo, Dar es Salaam leo, ikiwa ni mkakati wake wa ushirikiano na jamii wa kuendeleza elimu ya TEHAMA kwenye shule za sekondari.
Rodina Kimaro, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Songoro Mnyonge akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa komputa.

Na mwandishi wetu
KATIKA mkakati wa kuimarisha mafunzo ya TEHAMA nchini, Shule ya Sekondari ya Songoro Mnyonge na Kituo kinachosaidia Wajane na Watoto (CWCA), wamepokea msaada wa kompyuta zenye thamani ya Sh milioni 35.

Msaada huo uliotolewa na Benki ya Diamond Trust (DTB) kwa kushirikiana na taasisi ya ARISE ni miongoni mwa mikakati ya ushirikiano wa benki na jamii katika kuendeleza elimu ya TEHAMA kwenye shule za sekondari.

Kituo cha Kukuza Elimu cha Lauren (LEPC) ni miongoni mwa wanufaika wa msaada uliotolewa na DTB pamoja na ARISE.

Akizungumza wakati wa makabidhiano jana Jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki Ravneet Chowdhury, amesema mpango wao ni kujikita katika kuondoa uchafuzi wa mazingira kwa kutupa uchakavu utokanao na shughuli za mazingira ifikapo mwaka 2030.

“Kupitia mpango huu benki imeweka mipango mbalimbali ya urejelezi wa vifaa mbalimbali vya ofisi vilivyotumika kwa mfano kompyuta, simu n.k.Vifaa hivyo baada ya urejelezi wa hali ya juu hurudishwa kwa matumizi ya kufundishia TEHAMA katikashule mbalimbali,” amesema.

Ameongeza: “Tunajivunia kuweka maziungira yetu safi kwa kurejeleza kompyuta hizi ili ziweze kutumika mashuleni.”
Kwa mujibu wake, DTB na ARISE haijajikita tu katika usimamizi wa mazingira na utawala bora kama inavyoainishwa ndani ya mipango mikakati ya Umoja wa Mataifa ya kufikia malengo ya karne, bali pia ni uwakilishi wa maadili yetu ya kibiashara yanayoambatana na kulinda rasilimali zetu kwa ajili ya vizazi vijavyo na kuwawezesha kielimu.

Uday Bhasin, mnahisi wa ndugu watatu- Inaya Bhasin, Simar Bhasin na Rania Bhasin amesema ‘Arise’ ni asasi iliyojikita katika kauli mbiu ya ‘Kuwezesha, kuelimisha na kuifadhi.’

Katika ulimwengu wa ushindani kati ya wenye nacho na wasio nacho, ndugu hawa kwa msaada wa washauri mbalimbali walianzisha shirika la ARISE ikiwa na lengo la kusaidia mipango endlevu ya jamii.

“Katika jamii yenye ushindani , upungufu wa rasilimali na kuongezeka kwa idadi ya walionavyo na wasionavyo, wadada wa Bhasin wanaamini katika kuwainua waliokata tamaaa na kuwapa matumaini kwa kuwezesha program endelevu na zenye tija,” amesema Bhasin.

Utti Mwang’amba, mkurugenzi mtendaji katika Kituo cha kusaidia Wajane na Waatoto (CWCA) amesema Kituo hicho kinaamii kuwa msaada huo utachochea kazi zao za kila siku ikiwemo kuwawezesha wazazi ili waweze kuhudumia Watoto wao likiwepo suala la kuwapatia elimu.

“Tumekuwa tukipinga ndoa za utotoni na asilimia kubwa tumekuwa tukiwawezesha wazazi ili wapate mitaji ya kuudumia watoto wao hasa wa kike kwa kuwapeleka shule. Tunaamini kuwa msaada huu wa kompyuta utaongeza ujuzi wa TEHAMA hususani katika shule zisizo na vifaa hivyo,” amesema.
Akizungumza kwa niaba ya Afisa Elimu wa Wilaya ya Kinondoni, Explancer Siame Afisa wa Elimu ya Watu Wazima ameziomba taasisi hizo kuendeleza ari hiyo kwa shule nyingine za Manispaa, Wilaya na Mkoa kwani wapo wanafunzi wengi wenye uhitaji wa kompyuta.

“Tunatambua huu ni msaada wa kiroho endelezeni ubunifu huu,” ameongeza.

Rodina Kimaro, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Songoro Mnyonge, amesema msaada huo utarahisisha mzigo wa ufundishaji kutokana na shule kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi kuliko walimu waliopo.

“Tuna wanafunzi 1,300 na walimu 19. Ufundishaji sio mrahisi. Kupitia msaada huu tunaamini kwa njia moja ama nyingine utawapunguzia walimu mzigo wa kufundisha,” amesema Rodina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...