Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje amesema CATC ni moja ya vyuo vinavyotoa kozi ya Usalama wa Usafiri wa Anga (ASTC) na ni moja kati ya vyuo tisa vyenye sifa hizo Afrika na 35 duniani.

Mkuu wa Chuo Kanje ameyasema hayo akizungumza na watangazaji wa Radio Uhuru FM 95.7 Machi 19, 2024 Dar es Salaam katika kipindi cha Hello Tanzania.

Akiunganisha na mafaniko ya miaka mitatu ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan madarakani, Mkuu wa Chuo Kanje alisema CATC ni mnufaika na imepatiwa eneo ambalo linatarajiwa kujengwa majengo na miundombinu ya kisasa ya chuo pamoja kugharamiwa Ujenzi wake ambao ni takriban shilingi bilioni 78. Na kuongeza kuwa tayari serikali imeshatoa shilingi bilioni 5 na Ujenzi huo utakamilika ndani ya miaka mitatu.

Chuo cha CATC kimelenga zaidi kutoa kozi za muda mfupi zinazoanzia siku moja hadi mwaka mmoja katika maeneo ya Usimamizi wa Uongozaji Ndege, Usimamizi wa Utoaji Tarifa za Usafiri wa Anga, Uhandisi wa Mitambo ya Kuongozea ndege, Usalama wa Usafiri wa Anga, Uendeshaji wa Viwanja vya ndege, Ufundishaiji wa wakufunzi wa usafiri wa anga, Usimamizi wa Usafiri wa Anga pamoja na kuandaa kozi mbalimbali kuendana na mahitaji ya wateja.

Kwa upande wa mafunzo amesema Chuo hicho cha CATC kinatoa mafunzo kwa nchi zaidi ya 17 za Afrika.
Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga Tanzania (CATC) Aristid Kanje akiwa kwenye picha ya pamoja na Watangazaji wa Radio Uhuru FM pamoja na Afisa Habari Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga CATC Ally Changwila  mara baada ya kumaliza mahojiano katika kituo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...